WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Hawa Ghasia ameziagiza Halmashauri na Jiji la Dar es Salam
kujadiliana na kupata sheria nakanuni zitakazo ainisha utendaji kazi wao.
Kauli hiyo ilitoa jijini jana,
na waziri huyo, wakati akifungua mkutano wa wabunge na madiwani, wa mkoa
huo, kwa ajili ya majadiliano, kuhusu mustakabali wa jiji hilo.
Ghasia alisema kutokana na
mkanganyiko wa kazi za Mamlaka ya Jiji na zile za Halmashauri
kutoeleweka, mnapaswa kujadiliana hususan kuboresha sheria na kanuni
zake ili kuimarisha mahusiano, kupata sheria na kanuni zitakazo
tambulisha mipaka ya mamlaka hizo mbili kiutendaji.
Akizungumzia mradi wa Mabasi ya
endayo haraka (DART), alisema lengo la mradi huo, ni kuwa na usafiri
bora wa Umma wenye gharama nafuu, unaotumia mabasi makubwa.
Ghasia alisema dhima ya Mradi
huo ni kutoa huduma bora na nafuu jijini na kuleta ukuaji wa uchumi
endelevu kwa wananchi na kuwa kichocheo baina ya Serikali na Sekta
binafsi katika nyanja ya usafirishaji wa umma jijini.
Mwenyekiti wa Kamati ya DART, Dk
Didas Masaburi ambaye pia ni Meya wa Jiji hilo, alisema wanatarajia
kukihamishia Mbezi Luis kituo cha mabasi yaendayo mokoani na nje ya nchi
ifikapo Januri 15, 2013 ili kupisha mradi huo wa DART.
Alisema kwa kuwa mradi huo ni wa
wananchi, hivyo kuanzia sasa ushiriki wa madiwani na wenyeviti utapewa
kipaumbele lengo likiwa ni kuwafikisha wananchi elimu kuhusu umuhimu wa
mradi huo katika jamii.
Naye Diwani wa Kata ya Saranga
(Chadema), Efraim Kinyafu alisema wakati ujenzi huo, bado hakuna juhudi
za makusudi za kupanua barabara ili kuepuka foleni katika eneo la kimara
hadi kituo kipya cha Mabasi Mbezi.
Mkutano umependekeza maazimio
tisa yakiwemo ya, mkutano kati ya Meya wa Jiji na madiwani wa
halmashauri kufanyika mara mbili kwa mwaka, kuundwa kamati
itakayosimamia uandaaji sheria na kanuni zitakazo ongoza mamlaka hizo na
mengineyo ambayo yatajadiliwa katika mkutano utakaofanyika hivi
karibuni.
Akifunga Mkifunga Mkutano huo,
Naibu Katibu Mku (Tamisemi), Jumanne Mgini, alisema viongozi hao
wanapaswa kutambua kuwa suala la maendeleo yamo mikononi mwao, hivyo ni
bora kila wanapojadili maendeleo ya jiji hilo wanafikisha ujumbe sasa
hii kwa wananchi siyo vinginevyo.
Alisema suala la kuendeleza jiji hilo ni lao wenyewe hivyo wawe tayari kupokea machungu yatakayo ambatana na maendeleo.
No comments:
Post a Comment