CHELSEA
jana usiku iliweka rehani juhudi zake za kusaka ubingwa wa ligi kuu ya
Uingereza baada ya kuchapwa 1-0 na timu iliyopo mkiani, QPR.
Mchezaji
wa zamani wa Chelsea, Shaun Wright Phillips, ndiye aliyekuwa mwiba kwao
kufuatia bao lake la dakika ya 78 lililodumu hadi mwisho wa mchezo huo
uliofanyika katika dimba Stanford Bridge.
Shaun Wright Phillips baada ya kuitungua Chelsea
Kwa
goli hilo la Phillips aliyesaliwa na Chelsea mwaka 2005 kwa ada ya
pauni milioni 21 kutokea Manchester City, Kocha wa QPR Harry Redknapp
sasa anaamini amepata fomula ya kuinusuru timu yake na janga la kushuka
daraja.
“Ushindi
dhidi ya Chelsea ni ushindi bora zaidi katika maisha yangu ya soka”
alisema Redknapp ambaye timu yake ilipaki bus langoni mwake kwa muda
wote wa mchezo.
Mabao mawili ya Luis Suarez na moja la v Raheem Sterling yalitosha kuipa ushindi mnono Liverpool wa bao 3-0 dhidi ya Sunderland huku Newcatsle ikipokea kipigo cha 2-1 kutoka kwa Everton.
Luiz Suarez akichanja mbuga
wa Liverpool Daniel Sturridge akiufuatilia mchezo
Raheem Sterling akiifungia Liverpool bao la kwanza
Wakati
huo huo, Chelsea jana ilikamilisha usali wa mshambuliaji wa Newcastle,
Demba Ba kwa uhamisho wa ada ya pauni milioni 7.5 na mshahara wa pauni
75,ooo kwa wiki.
Demba Ba, kifaa kipya cha Chelsea
No comments:
Post a Comment