Msemaji rasmi wa vikosi vya jeshi la ulinzi la Misri amekadhibisha
habari iliyotangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa jeshi la nchi
hiyo limetumia silaha kuwakandamiza wafanya maandamano nchini humo.
Ahmad Muhammad Ali amekanusha habari iliyotangazwa na baadhi ya vyombo
vya habari kwamba jeshi la Misri limewafyatulia risasi waandamanaji huko
katika mji wa Port Said na kuwauwa raia wengi miongoni mwao. Msemaji wa
vikosi vya jeshi la ulinzi la Misri amesisitiza kwamba hakuna raia
yoyote wa Misri aliyeuliwa kwa kufyatuliwa risasi. Amevitaka vyombo vya
habari kuacha kutangaza habari zisizo sahihi kuhusiana na yale
yanayojiri huko Port Said. Watu 31 wameuawa na wengine 445 kujeruhiwa
katika mapigano yaliyotokea juzi Ijumaa huko Cairo na katika miji
mingine ya Misri.
No comments:
Post a Comment