Karibu watu wengine 200 wamejeruhiwa
katika moto huo uliotokea kwenye klabu ya Kiss katika mji wa Santa
Maria, kusini mwa Brazil.
Mkuu wa kikosi cha Zima Moto cha eneo
hilo, Guido de Melo, amesema kuwa, watu waliemewa na kuchanganyikiwa
wakati moto huo ulipoanza kuwaka.
Ajali hiyo inakumbushia majanga mengine
kama hayo yaliyowahi kuikumba Brazil katika miaka ya huko nyuma ambapo
watu 100 walipoteza maisha wakati klabu moja ya usiku ilipowaka moto
huko Rhode Island mwaka 2003 na wengine karibu 200 kufariki dunia baada
ya moto kuchoma klabu moja ya usiku mjini Buenos Aires mwaka 2004.
No comments:
Post a Comment