Uchunguzi uliofanywa na serikali
ya Afrika Kusini haukugundua ushahidi wowote kuwa fedha za taifa
zilitumiwa kujenga nyumba binafsi ya Rais Jacob Zuma - swala ambalo
limezusha utata kwa miezi kadha.
Lakini Waziri wa Ujenzi, Thembalani Thulas
Nxesi, aliwaambia waandishi wa habari kwamba zaidi ya dola milioni-7 za
serikali zilitumiwa kuimarisha ulinzi kwenye nyumba hiyo ilioko Nkandla.
Kati ya kazi hiyo ilikuwa kujenga pahala pa helikopta kutua, zahanati na nyumba za kuishi walinzi wa rais.
Uchunguzi huo uliamua kuwa Rais Zuma hakuwa na kauli katika mipango hiyo ya usalama.
No comments:
Post a Comment