WASANII
nyota wa muziki wa kizazi kipya, Diamond na Bob Junior, kwa siku chache
za hivi karibuni, wameweza kuchuana vikali katika kuachia nyimbo mpya.
Wasanii
hao wenye upinzani mkubwa wamekuwa ni kama waliokuwa wanategeana
kuachia nyimbo ambapo baada tu ya Diamond kupakua wimbo wake “Nataka
kulewa” , wiki chache baaadae Bob Junior akaachia “Kichuna”.
Kuona
hivyo, wiki moja baadae, Diamond akashuka na kitu kipya “Kesho” ambao
ulionekana kama umelepelekwa mahsusi kuuzima wimbo wa Kichuna.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, siku mbili baada ya wimbo wa Diamond, Bob Junior nae akaachia wimbo mpya “Kizembe”.
Diomond
ambaye nyimbo zake zilizomtoa zimepita kwenye mikono ya Bob Junior, kwa
muda mrefu amekuwa akitajwa kuwa ana bifu kali na producer wake huyo wa
zamani.
Haileweki
kama piga nikupige ya kuchia nyimbo mpya zitaaishia hapo au
zitaendelea, lakini wataalam wa muziki wanasema spidi hiyo haitawasaidia
kitu zaidi ya kuwamaliza.
Msanii mmoja mzoefu wa Bongo Fleva ameimbia Saluti5: “Ukiangalia nyimbo “Kesho” na “Kizembe” ni nyepesi sana, hazina jipya.
“Kwa
mfumo wa soko ulivyo, kuachia nyimbo mpya haraka haraka ni kujimaliza”
alisema msanii huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.
CHANZO CHA HABARI NA SALUTI 5
No comments:
Post a Comment