KATIKA safu ya mastaa wanaotawala kwenye midomo ya wapenzi wa filamu
za Bongo, jina la Jackline Wolper Masawe, ni miongoni mwa yanayovuma
kutokana na kazi zake mbalimbali alizofanya kai ya mwaka 2011 hadi sasa.
Baadhi ya mastaa aliowahi kuigiza nao ni pamoja na Steven Kanumba,
Wema, Ray, JB, Cloud na wengineo.
Bila shaka huko ndiko alikoonyesha
ufundi wa hali ya juu na kujizolea umaarufu mkubwa Tanzania, Kenya,
Uganda, Congo na kwingineko Afrika.
Mwaka 2012, Wolper aliingia katika skendo za hapa na pale, ijapokuwa hazikuwa mbaya sana, lakini zilihusu maisha yake binafsi kati yake na aliyekuwa mpenzi wake, Ramadhan Mtoro 'Dallas'.
Katika habari tofauti tofauti ukiachana na kupokonywa gari, kudaiwa kuwa na ugomvi na baadhi ya wasichana maarufu, kulikuwa na nyeti moja ambayo mpaka hivi sasa wengi walikuwa gizani.
Kauli mbalimbali zilizotolewa na watu wa karibu na mwigizaji huyo kuwa amebadili dini kwa mara nyingine na kuurudia ukristo, zimepingwa vikali na staa huyo huku akidai kuwa wanaomsingizia hivyo watoe ushahidi na si maneno matupu.
Licha ya baadhi ya watu kudai kuwa alishaonekana msikitini mara
kadhaa, huku bado akiendelea kuhudhuria kanisani, Wolper amesema kwa
kipindi fulani amekuwa akishutumiwa kwa mambo mengi yasiyo kweli.
Mwaka 2012, Wolper aliingia katika skendo za hapa na pale, ijapokuwa hazikuwa mbaya sana, lakini zilihusu maisha yake binafsi kati yake na aliyekuwa mpenzi wake, Ramadhan Mtoro 'Dallas'.
Katika habari tofauti tofauti ukiachana na kupokonywa gari, kudaiwa kuwa na ugomvi na baadhi ya wasichana maarufu, kulikuwa na nyeti moja ambayo mpaka hivi sasa wengi walikuwa gizani.
Kauli mbalimbali zilizotolewa na watu wa karibu na mwigizaji huyo kuwa amebadili dini kwa mara nyingine na kuurudia ukristo, zimepingwa vikali na staa huyo huku akidai kuwa wanaomsingizia hivyo watoe ushahidi na si maneno matupu.
Wolper anasema licha ya kwamba ameachana na mchumba wake Dallas, atabaki kuwa Muislam hadi mwisho wa maisha yake.
Wolper ambaye sasa anafahamika kwa jina la Ilham alisema, ni kweli alibadili dini baada ya kuchumbiwa na Dallas, lakini atakuwa anamchezea Mungu kama ataamua kurudi kwenye ukristo baada ya uchumba huo kuvunjika.
"Mimi nitabaki kuwa muislamu hadi kifo, siwezi kurudi kwenye ukristo kwani ninaupenda uislamu," alisema.
"Akitokea mwanaume muislamu akataka kunioa niko tayari na hata akija mkristo pia niko tayari kuolewa naye, ila nitaendelea kuwa muislamu,alisema Wolper aliyezaliwa Desemba 6, 1988 mkoani Kilimanjaro.
Wolper alibadili dini mwaka jana baada ya kuingia kwenye uhusiano na Dallas lakini hivi karibuni kulikuwa na madai kwamba amerudi kwenye ukristo.
"Ukweli halisi nitabaki kuwa nao mimi mwenyewe, kwani sijawahi kumchezea Mungu, ndugu jamaa na marafiki wanajua dini yangu, sasa hao watu ya karibu na mimi ni kina nani?" Alihoji.
Anafafanua kuwa yeye ni mtu wa namna tofauti na vile watu wanavyomdhania, kutokana na ukarimu alionao na jinsi anavyoendesha mambo yake akiwa kama msanii ambaye ni kioo cha jamii.
"Mimi ni msanii kioo cha jamii, najua nini napaswa kufanya, kiukweli kama umeangalia katika skendo nyingi wanazoziandika na kuzisambaza ni hazina ukweli wowote na mara nyingi hata picha ni za kutengeneza, sijawahi kuwa na skendo hayo yote ni kusingiziwa," anasema.
"Kama ni kweli skendo mimi inanihusu basi kuwe na picha mbele ya blogu au gazeti inayonionyesha mimi nikifanya kitendo tofauti na utamaduni wa Mtanzania.
"Lakini haya yote ni ndoto. Siwezi kusema hata wengine wanasingiziwa, hapana hapa najizungumzia kama Wolper maana najua nyendo zangu zote."
Anasema anachofikiria kufanya kwa sasa ni kuhakikisha filamu zake sita alizoshindwa kuzikamilisha mwaka jana, zinatolewa mwanzoni mwa mwezi Februari.
"Mwaka jana nilibakiza viporo sita, nimefanya kazi vizuri sana na nawahakikishia Watanzania wataridhika na kazi yangu," anasema mwigizaji huyo anayemiliki kampuni ya utayarishaji wa filamu ya Lain Wolper.
"Lakini nilichelewa kidogo kuzitoa na mwishoni mwa wiki hii zitakuwa sokoni. Yaani ninafanya kazi na kampuni nyingi zikiwamo Papazi, Steps na nyinginezo.
"Nimefungua kampuni yangu toka mwaka jana, kiukweli sikuweza kuitangaza kutokana na kukosa ubora ule ninaouhitaji mimi, najitahidi ili mwaka huu niweze kuiboresha zaidi, na hiyo ndiyo mikakati yangu kwa mwaka 2013."
Wolper ambaye amejizolea umaarufu, anakiri kuwa hajawahi kutoka nje na Tanzania, hivyo mwaka huu anajipanga kufanya ziara nje na amepanga kuanzia Kenya.
"Nina ndoto ya kufanya kazi na wasanii wa nje ya Tanzania, ninajipanga zaidi katika hili, nadhani wasanii tunapaswa kuwa na maono ya mbali," anabainisha.
Wolper hivi sasa anaandaa filamu mpya atakayoshirikiana na msanii maarufu, Elizabeth Michael 'Lulu', ambaye mwanzoni mwa wiki hii alitoka rumande baada ya kupata dhamana katika kesi inayomkabili.
Tangu Aprili mwaka jana, Lulu alikuwa rumande akikabiliwa na kesi ya tuhuma za kuua bila kukusudia, anatuhumiwa kumuua msanii,Steven Kanumba.
Akizungumzia filamu hiyo, Wolper alisema anatarajia itafanya vizuri sokoni.
"Nimeshampokea Lulu tangu moyoni mwangu kwani kule alikokuwepo si sehemu nzuri na ukiangalia bado ni mtoto mdogo hivyo inaumiza sana," anasema.
Filamu hiyo ndiyo itakayokuwa ya kwanza kuchezwa na Lulu baada ya kufika uraiani.
Habari na HERIETH MAKWETTA wa Mwanasport.
No comments:
Post a Comment