WASHINGTON, Marekani
IDADI kubwa ya wanawake wamekuwa wakifanya
upasuaji wa viungo vyao vya mwili ili kuwa na mvuto pamoja na mwonekano
wa tofauti barani Ulaya na Marekani.
Lakini sasa hata wanaume wametumbukia katika mtego huo wa kutaka kubadili sura au viungo vingine vya miili yao.
Lakini sasa hata wanaume wametumbukia katika mtego huo wa kutaka kubadili sura au viungo vingine vya miili yao.

“Siku zote nimekuwa nikifanyiwa upasuaji huu kwa sababu nilikuwa ni mtu mbunifu wa kutaka kubadilika zaidi,” Jedlica anasema katika mahojiano kwenye Shoo ya The Doctor, inayoonyeshwa kupitia televisheni nchini Marekani.
Katika baadhi ya upasuaji wake kulikuwa na upasuaji wa mifupa, fuvu la kichwa, mashavu, midomo, kidevu na makalio.
Alianza kufanyiwa upasuaji huo alipokuwa na umri
wa miaka 18, awali kabisa aliwahi kukumbwa na balaa wakati alipofanyiwa
upasuaji wa pua.
“Ni kweli hicho ni kitu ambacho kilikuwa kinaniweka mbali sana na watu wengi mpaka pale wengine wakasema kuwa ningekufa katika upasuaji,” alisema baada ya kufanyiwa upasuaji na kubadilika sura yake kwa kiasi kikubwa.
Alijigamba kuwa ameweza kugharamia upasuaji wake
huo yeye mwenyewe, kwa kutangaza bidhaa mbalimbali kupitia shati
alilovaa pamoja na kutumika na wanamitindo mbalimbali wakati wa shoo za
mavazi.
Licha ya kupasuliwa, Jedlica pia ametumia madawa mbalimbali aina ya silicone katika kutunisha ukubwa wa makalio yake ili kuweza kupata mwonekano aliokuwa akiuhitaji.
Jedlica anasema kuwa anahisi upasuaji huo ni njia ambazo anaweza kujitibu mwenyewe.
“Ni kama vile ninavyoweza kujitibu mwenyewe kwa kujichonga na kufanya mchoro mimi mwenyewe,”alisema.
Ingawa wafanyakazi na madaktari mbalimbali
walioangalia kipindi hicho walifanya majadiliano na kuonyesha wasiwasi
kuhusu idadi ya juu ya upasuaji wa Jedlica, madaktari hao walimtaka
Jedlica aache mara moja kufanyiwa upasuaji, hata kama hiyo ni haki yake.
Mmoja wa madaktari alisema kuwa wakati Jedlica
anaona ni ufahari mkubwa kufanyiwa upasuaji, amekuwa na bahati ya
kuepuka hatari nyingi katika kazi ya upasuaji wake wote zaidi ya mara
90.
Hata hivyo walisema kuwa Jedlica kwa sasa ameshaishiwa chembe hai mwilini kutokana na upasuaji huo wakitahadharisha kwamba anaweza kupoteza maisha wakati wowote.
Hata hivyo walisema kuwa Jedlica kwa sasa ameshaishiwa chembe hai mwilini kutokana na upasuaji huo wakitahadharisha kwamba anaweza kupoteza maisha wakati wowote.
“Kuna kila dalili ya mambo mengi kwenda vibaya, lakini hatari kubwa ni namna alivyouharibu mwili wake, “ anasema.
Lakini Jedlica anasema: “Nimekubali kukutana na rizki hizi,
lakini naamini hakuna kitu katika maisha kinachokuwa na mafanikio bila
kukabiliana na hatari maishani.”
Herieth Makwetta kwa msaada wa mtandao
No comments:
Post a Comment