KATIKA mkakati wa kusambaza mawasiliano
ya mfumo mpya wa dijitali katika mikoa 14 nchini, jumla ya Sh50 milioni
zimetolewa na Kampuni ya StarTimes ili kuwezesha kazi hiyo.
Meneja Habari wa StarTime, Erick David aliitaja
mikoa ambayo kampuni hiyo imewekeza kuwa ni pamoja na Shinyanga, Iringa,
Tabara, Ruvuma, Mara, Kigoma na Manyara.
Mikoa mingine ni Singida, Kusini Pemba, Kaskazini Pemba na Rukwa, Mtwara na Lindi na kwamba mikoa 23 inatarajia kupatiwa huduma hiyo kufikia mwisho wa mwaka huu.
“Huduma hii ya kukodisha ving’amuzi ni mpya
kutoka Startimes, kutatua changamoto zinazoikabili dijitali na kwamba
mteja anatakiwa kutoa Sh39,000 kama dhamana ya kuchukua king’amuzi na
pia mteja anatakiwa kulipa Sh6,000 kama malipo ya kila mwezi na
itakuwa na chaneli 15 za nyumbani na nyinginezo,” alisema David.
Alisema mteja anaweza kurudisha na akarudishiwa Sh39,000 aliyotoa kama dhamana baada ya matumizi yake na huduma hiyo inayolenga kuwanufaisha watu wa kipato cha chini kwani licha ya kukodishwa utapata channel zaidi ya 15 saa 24 kwa mwezi mzima.
Alisema katika kuifanya jamii kuwa karibu na
ulimwengu huu wa dijitali na kuepuka gharama kubwa za ununuzi wa
ving’amuzi na malipo ya vifurushi kwa kila mwezi kampuni yao
inarahisisha hilo.
No comments:
Post a Comment