Mwenyekiti
wa UVCCM Taifa Ndg Sadifa ametengua uteuzi wa wajumbe wa baraza ambao
alikuwa amewateua Ndg Paul makonda pamoja na Msaraka , Makonda katolewa
kikaoni sasa hivi kwa kuwa uteuzi umetenguliwa kaambiwa sio mjumbe tena
awapishe kikaoni!! UVCCM tutafika kweli , guy hii sio bure tumerogwa
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) unafanya kikao chake
cha kwanza cha Baraza Kuu la Umoja huo, ambapo ajenda mbalimbali
zitajadiliwa ikiwemo tathmini juu ya Hali ya Vijana na Siasa Nchini,
lakini pia tathmini ya sehemu ya mkakati wa maamuzi ya Mkutano Mkuu
ikiwemo mikakati ya kuimarisha Chipukizi na Uhamasishaji.
Pamoja na hayo, kutajadiliwa pia mikakati ya kiuchumi ya kuiwezesha
jumuiya ya Umoja wa Vijana kujitegemea kiuchumi kwa kuweka mipango imara
ya uzalishaji ili kukuza mapato ya jumuiya. Kikao kitajadili miradi
iliyopo na muendelezo wake lakini pia kutafakari juu ya kuanzisha miradi
mipya ya jumuiya hiyo.
Kikao hicho kitafanya Uteuzi wa Baraza la wadhamini wa UVCCM pamoja na
Kamati ya utekelezaji, kisha kitamalizika kwa semina kwa wajumbe wa
Baraza Kuu la UVCCM Taifa juu ya wajibu na majukumu ya wajumbe wa Baraza
na kukumbushana juu ya majukumu na wajibu wa jumuiya ya UVCCM katika
kuimarisha Uhai wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya shina hadi Taifa.
No comments:
Post a Comment