EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, February 17, 2013

MKURUGENZI MKUU WA ELIMU NCHINI AJIUZULU

Kufuatia sakata kuwa Serikali haina mitaala rasmi ya kufundishia shuleni, Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania, Dk Paul  Mushi,  amejiuzulu wadhifa huo.
Picture
Dk Mushi

Nafasi yake imechukuliwa na  Mkurugenzi wa Idara ya kubuni  na kuendeleza Vifaa vya Elimu, Dk Leonard Akwilapo.

Akihojiwa na  NIPASHE kwa njia ya simu jana jijini Dar es Salaam,  Dk. Mushi alithibitisha kujiuzulu na kusema alichukua hatua hiyo kwa hiari yake   bila kushinikizwa na mtu, “Hakuna aliyenishinikiza nimeamua mwenyewe kuandika barua ya kujiuzulu,” alisema Dk Mushi

Kaimu Mkurugenzi Dk Akwilapo alipohojiwa juu ya mtangulizi wake   aliyeachia ngazi , Alhamisi wiki hii, alisema aliondoka kwa maamuzi yake mwenyewe bila shinikizo kama alivyoeleza, “Sio siri ni kweli amejiuzulu na aliniambia ni maamuzi yake aliyoyafanya ya kujivua madaraka ya Mkurugenzi Mkuu bila ya kugombana na mtu na juzi ndio alipewa barua yake na mimi kupatiwa barua ya kuwa kaimu,” alisema Dk Akwilapo
Katika mkutano wa  Bunge la mwezi huu, Mbunge wa kuteuliwa na Rais  James Mbatia (NCCR-Mageuzi),  aliwasilisha bungeni hoja binafsi kuhusu udhaifu uliopo katika sekta ya elimu hapa nchini.

Katika hoja hiyo, alilaumu kutokuwapo kwa  mitaala inayoongoza ufundishaji wa masomo shuleni hali inayosababisha kudorora kwa elimu. Kadhalika  aliibua tuhuma za uchapishwaji wa vitabu ambavyo maudhui  yake hayana viwango pia waliopewa kazi ya kuchapisha ndiyo hao waliokuwa wahariri na waandishi. Pia alihoji sababu za uchapishaji wa vitabu hivyo  kufanyika nje  ya Tanzania hali ambayo inasababisha kuwapo kwa matumizi mabaya ya fedha.

Katika kujibu hoja hizo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi alilithibitishia Bunge kuwa serikali ina mitaala na nakala zake ziliwasilishwa bungeni  na hoja hiyo ikazimwa. Baada ya kuwasilishwa kwa mitaala hiyo, bunge iliunda kamati ya kujiridhisha kama ni kweli mitaala hiyo ni sahihi ambapo ilikuja na majibu ya kujiridhisha kuwa ni ya kweli.

Hata hivyo, kwa upande wa James Mbatia alisema bado kuna utata katika mitaala hiyo licha ya kamati hiyo kujiridhisha kuwa mitaala ipo sahihi.
via gazeti la NIPASHE

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate