WANAFUNZI wawili wa Shule ya Msingi Mjimpya, wilaya ya Temeke,
jijini Dar es Salaam, wamekufa baada ya kugongwa na gari lenye namba za
usajili T 324 APW aina ya Canter.
Kamanda wa polisi, mkoa wa Temeke Engribert Kiondo, alisema kuwa
ajali hiyo ilitokea juzi saa 11 jioni huko barabara ya Temeke eneo la
Pile, ambapo dereva wa gari hilo, ambaye hakufahamika, akitokea Temeke
Mwisho kuelekea kwa Azizi Ally, alishindwa kulimudu na hatimaye kuacha
njia na kuwagonga watoto hao na kufariki papo hapo.
Aliwataja wanafunzi hao kuwa ni Hassan Yusufu (8) wa darasa la pili na Amour Yusufu (6) wa darasa la awali katika shule hiyo.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke.
Wakati huohuo, moto ulizuka ghafla katika kiwanda cha Cotex maeneo ya
Mbezi Jogoo, kinachotengeneza bidhaa za vipodozi na miswaki na
kuteketeza mali zote zilizokuwemo ndani na baadhi ya mitambo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela,
tukio hilo lilitokea juzi saa 12 jioni na kwamba chanzo cha moto huo
inasadikiwa ni hitilafu ya umeme. Thamani ya mali iliyoungua bado
haijafahamika.
No comments:
Post a Comment