EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, February 16, 2013

Wassira, Mwema watimuliwa..Mauaji ya mchungaji Geita

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, wametimuliwa mkoani Geita, huku Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, akisulubiwa kwa masharti magumu.

Vigogo hao wa serikali walikumbwa na patashika hiyo, juzi mkoani humo walikoenda kusaka suluhu ya vurugu za kidini zilizosababisha mauaji ya Mchungaji Mathayo Kachila (45) wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God.

Habari za uhakika kutoka mkoani Geita zimesema kuwa mamia ya wananchi wa Geita walitishia kufanya lolote, ikiwa Wassira na Mwema wangeonekana wakati wa mazishi ya mchungaji huyo au sehemu yoyote mkoani humo.

Taarifa za uhakika zimesema kuwa viongozi wa wilaya na mkoa huo, baada ya kubaini kuwepo na hali ya hatari kwa viongozi hao, walilazimika kubadili eneo ambalo helkopta iliyowabeba mawaziri na IGP ingetua.

Uchunguzi umebaini kuwa, chopa hiyo, awali ilitua katika eneo la Kalangalala, lakini baada ya kubainika kuwepo na hali ya hatari, ililazimika kuruka na kwenda kutua katika eneo la Magereza mjini Geita.Mawaziri hao waliandamana na Mwema, toka Dodoma kulikokuwa kunafanyika kikao cha makamishna wa polisi, makamanda wa mikoa na Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa wakazi wengi wa mjini Geita, hususan Wakristo, walipata taarifa ya ujio wa mawaziri hao, ndipo walipoamua kuchukua hatua hizo, na kwamba wasingekuwa tayari kuonana na Wassira kwa madai kuwa alitoa tamko lililochochea zaidi chuki baina ya waumini wa dini ya Kikristo na Kiislamu, huku wakimshutumu IGP Mwema kwa kuzembea kuchukua hatua kulinda usalama wa watu.

Kutokana na hali hiyo, ilimlazimu Waziri Nchimbi kutumia juhudi kubwa kuwashawishi wananchi wakubali kumsikiliza kwa nia ya kupata ufumbuzi wa vurugu hizo.
Imedaiwa kwamba Nchimbi alikubaliwa kuonana na wananchi ambao walimpa masharti mazito matano aliyolazimishwa kuyakubali, kama njia ya kupata ufumbuzi.
Sharti la kwanza alilopewa, walimtaka akubali na kutamka hadharani kuwa serikali haina dini, na hivyo sio lazima kwa Waislamu tu ndio wachinje na Wakristo wasichinje.

Sharti la pili ambalo Nchimbi alipewa na kulitekeleza hapo hapo ni kuwaachia wachungaji waliokuwa wamekamatwa kwa madai ya kuchinja, wakati sharti la tatu lilimtaka athibitishe kuwa wachungaji na Wakristo wengine wataacha kunyanyaswa na Waislamu.
Sharti la nne lilimtaka Nchimbi atamke kuwa serikali itagharamia matunzo ya familia ya mchungaji aliyeuawa na mazishi yake kwa sababu kifo chake kimetokana na uzembe wa serikali kutochukua hatua dhidi ya jambo hilo pamoja na kulalamikiwa na kupewa taarifa na wachungaji kwa barua.

Hata hivyo, Nchimbi aliomba jambo hilo hususan matunzo ya familia aliwasilishe kwa wakubwa wake wa kazi, hususan Waziri Mkuu ili waweze kupata ufumbuzi wa pamoja.
Pamoja na juhudi hizo za Nchimbi, Mkuu wa Mkoa Saidi Magalula, na Mkuu wa Wilaya Ludorick Mpogolo, walikataliwa kabisa na wananchi, kiasi cha kushindwa kuhudhuria mazishi ya mchungaji huyo. Mashuhuda waliokuwepo kwenye msiba huo, wanasema Mpogolo aliyekuja kwa niaba ya serikali alizomewa hali iliyomsababisha atoe rambirambi haraka na kuondoka eneo la tukio.
Taarifa zaidi zilizopatikana zinasema Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kufika Geita leo ili kutafuta suluhu ya madhehebu hayo.

Wakazi wa kata za Buseresere na Katoro katika wilaya za Chato na Geita walilalamikia serikali kushindwa kutoa msimamo juu ya mgogoro huo na kuufanya wa kisiasa zaidi jambo lililosababisha vurugu na mauaji ya mchungaji na baadhi ya raia kujeruhiwa vibaya.
Katika vurugu hizo, mali za wananchi zimeharibiwa vibaya huku baadhi ya maduka na bidhaa zikiteketezwa kwa moto.

Miongozi mwa wananchi walioharibiwa mali zao ni pamoja na Mwenyekiti wa BAKWATA Wilaya ya Chato na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Buseresere, Yusuf Idd Banana ambaye ametaja mali zilizoharibiwa kuwa na thamani ya sh milioni 10.
Waziri Nchimbi hakupatikana kwa simu kuzungumzia hali hiyo kwa kuwa simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate