MKAZI wa Kijiji cha Itunge wilayani Kyela, Asanga Mwandepu (67) amefukua
kaburi la mwanamke katika kijiji cha Kingila, akachukua nguo za
marehemu na kuzitundika juu ya mti na kulima tuta la viazi kwenye kaburi
hilo. Inadaiwa katika kaburi hilo alizikwa mwanamke Basikaja Nkemwa
miaka mitatu iliyopita.
Akielezea tukio hilo mtoto mkubwa wa marehemu, Semu Mwakalebela alisema wazazi wake wote wamekwisha kufariki dunia.
Semu alisema alishangazwa na kitendo alichokumbana nacho cha kukuta kaburi la mama yake likifukuliwa na mfukuaji akitoa nguo za marehemu na kuzitundika juu ya mti.
Alisema alipiga mayowe kuomba msaada kwa majirani ambao walifika na kujionea kitendo hicho wakamkamata mtu huyo na kumfikisha kwenye ofisi ya serikali ya kijiji kabla ya kumfikisha polisi.
“Nashangazwa na kitendo hiki kwa maana mtu huyu analifahamu fika kaburi la mama yangu na hata yeye alishiriki katika mazishi hayo… sijui ni kipi kilichomsibu hadi kufikia uamuzi hao mgumu,’’ alisema Mwakalebela.
Mmwenyekiti wa Kijiji cha Kingila,
Gwandumi Mwaipyana alisema serikali ya kijiji iliamua kumfikisha
mtuhumiwa polisi ili sheria ifuatemkondo wake.Akielezea tukio hilo mtoto mkubwa wa marehemu, Semu Mwakalebela alisema wazazi wake wote wamekwisha kufariki dunia.
Semu alisema alishangazwa na kitendo alichokumbana nacho cha kukuta kaburi la mama yake likifukuliwa na mfukuaji akitoa nguo za marehemu na kuzitundika juu ya mti.
Alisema alipiga mayowe kuomba msaada kwa majirani ambao walifika na kujionea kitendo hicho wakamkamata mtu huyo na kumfikisha kwenye ofisi ya serikali ya kijiji kabla ya kumfikisha polisi.
“Nashangazwa na kitendo hiki kwa maana mtu huyu analifahamu fika kaburi la mama yangu na hata yeye alishiriki katika mazishi hayo… sijui ni kipi kilichomsibu hadi kufikia uamuzi hao mgumu,’’ alisema Mwakalebela.
Alisema awali wazee wa mila wa kijiji hicho walikaa baraza lao na kumtaka mtuhumiwa huyo kutozwa faini ya Sh 400,000 kama adhabu lakinihakuwa na kiasi hicho lakini serikali ya kijiji ilishauri jambo hilo lishughulikiwe kisheria.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kajunjumele, Imani Mwailunga alisema suala hilo limeachiwa serikali kwa hatua za sheria.
No comments:
Post a Comment