EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, March 25, 2013

Aliyechoma watoto wake midomo jela miaka 5

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro imemhukumu kifungo cha miaka mitano jela, Jaribu Juma (29), baada ya kupatikana na hatia ya kujeruhi na kufanya ukatili dhidi ya watoto.

Hukumu hiyo iliyotolewa huku mshtakiwa huyo akiwa hana ndugu hata mmoja aliyefika mahakamani hapo kushuhudia, imetolewa na Hakimu wa mahakama hiyo, Godfrey Isaya, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mawakili wa Serikali, Sunday Hyera na Akisa Mhando.
                                      Kamanda wa Polisi Morogoro, Faustine Shilogile.
Katika shtaka la kwanza la kujeruhi mtoto wa kwanza, mshtakiwa huyo alihukumiwa kwenda jela miaka minne, vivyo hivyo kwa kosa la pili, la kujeruhi mtoto wa pili, ambapo amehukumiwa adhabu kama hiyo ya miaka minne, huku kosa la tatu la ukatili dhidi ya mtoto akihukumiwa kulipa faini ya shilingi laki tatu, au kwenda jela miaka mitano, na kwa kosa la nne la ukatili dhidi ya mtoto mwingine, akipewa adhabu kama hiyo.

Hata hivyo, akifafanua hukumu hizo, Hakimu Isaya alisema kuwa mshtakiwa akiamua kutumikia adhabu zote kwa kifungo cha jela, adhabu hizo zote zitakwenda sambamba, hivyo atatumikia kifungo cha miaka mitano jela, na kwamba iwapo atalipa faini kwa kosa la tatu na la nne, basi atakwenda jela miaka minne.

Hakimu Isaya alisema mshtakiwa ana haki ya  kukata rufaa ndani ya siku 30 tangu hukumu kutolewa.
Kabla ya kutoa adhabu hizo, alisema mahakama imezingatia kuwa mshtakiwa ni baba wa watoto hao, na hilo ni kosa lake la kwanza, lakini ni baba aliyegeuka hatari kwa watoto wake na kujenga malezi na makuzi mabaya dhidi yao, tabia ambayo sio nzuri kwa wazazi na imekuwa ikijitokeza sana kwa jamii hivyo haipaswi kuachiwa.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Machi 13, mwaka huu, ambapo bila halali na kwa kujua kufanya hivyo ni kosa kisheria, aliwachoma moto midomo watoto wake wawili, Malick Jaribu (5) na Ibrahim Jaribu (10) baada ya kuwatuhumu kula karanga walizoachiwa kwaajili ya kuuza.

Kabla ya hukumu hiyo, mshtakiwa huyo alizua tafrani mahakamani, baada ya kugoma kuingia kwenye chumba cha mashtaka kusikiliza hukumu, ambapo alijiangusha chini na kujigalagaza, jambo lililowalazimu askari polisi kuingilia kati na kumnyanyua mshtakiwa huyo hadi ndani.

Aidha akijitetea kabla ya kutolewa hukumu hiyo, mshtakiwa huyo aliiomba mahakama kumuonea huruma kwa vile alikuwa ni baba wa familia, na tegemeo kwa watoto wake ambao amedumu nao kwa zaidi ya miaka minne sasa, na kuomba mahakama iwapo itabaini kurudia tena kosa kama hilo, impe adhabu kali ili iwe fundisho kwake na kwa wengine.

“Mheshimiwa hakimu, sikudhamiria kufanya hivi na ndio maana nimemua kukiri mbele hya baraza lako tukufu, lakini siwezi kusema mengi, mahakama itoe tu adhabu itakavyoona ili iwe fundisho kwangu na kwa wengine,”alisema mshtakiwa huyo ambaye awali aliomba mahakama kumuonea huruma kwa vile kosa hilo lilikuwa ni la kwanza.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate