Akizungumza Jumamosi jijini Dar es Salaam, jana, Rais
wa CWT, Gratian Mkoba, alisema endapo serikali haitaidhinisha madai yao
ni lazima moto uwake kwani wamechoka kufanya kazi katika mazingira
magumu na kudharauliwa.
Rais wa CWT, Gratian Mkoba.
Chama cha Walimu nchini (CWT) kimetishia kuwasha moto mpya iwapo serikali itaendelea kupuuzia madai ya stahili zao.
Hayo ameyabainisha wakati kamati ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda,
ikichunguza sababu za wanafunzi kufanya vibaya kwenye mtihani wa kidato
cha nne mwaka jana na kusisitiza kuwa hawatafuata sheria na
'patachimbika'.
Alisema endapo bajeti ya mwaka huu itapita bila kutekeleza ahadi za
nyongeza ya mishahara ya walimu kama walivyokubaliana siku za nyuma,
hawatakuwa na sababu za kufuata utawala wa sheria wala chochote kwa kuwa
serikali yenyewe haifuati sheria.
“Huu utakuwa ni mgogoro mpya endapo bajeti ya mwaka huu itapita
bila kuongeza mishahara ya walimu ni lazima moto utawaka na wabunge
waiulize serikali madai ya walimu yamefikia wapi na tutaendelea kuteseka
hadi lini,” alisema.
Aliwataka wabunge kuiuliza serikali juu ya nyongeza ya mshahara wa walimu ikiwa ni jitihada za kuboresha elimu nchini.
Kuhusu Kamati ya Pinda, ana hofu kuwa serikali ina nia mbaya na
walimu kwani kitendo cha hivi karibuni cha kuunda kamati ya Waziri Mkuu
bila kutaja chochote juu ya kuchunguza marupurupu na nyongeza ya
mishahara ya walimu kunawaacha vinywa wazi.
Mkoba alisema madai yao sio mapya yanafahamika na kwamba kama serikali imeyasahau watarudi mahakamani kuikumbusha.
Alisema Agosti mwaka jana walifanya mgomo wa kutaka nyongeza ya
mshahara ifikie asilimia 100, posho ya kufundishia asilimia 55 kwa
walimu wa sayansi na wa sanaa ifikie asilimia 50. Kingine ni asilimia 30
ya posho ya mazingira magumu jambo ambalo mpaka sasa halijatekelezwa.
Mkoba alisema shauri lao lilipelekwa mahakamani na kuamulikwa kuwa
serikali pamoja na walimu wake kulijadili lakini serikali haijawahi
kukubaliana na hatua hiyo licha ya kwamba mwisho wa kulijadili kisheria
suala hilo ilikuwa Desemba 5 mwaka jana.
Ukosefu wa walimu, upungufu wa vitabu na mazingira duni ya
kujifunzia ni baadhi ya sababu zilizotolewa na wadau wa elimu
waliohojiwa na tume ya kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka
2012
No comments:
Post a Comment