MWIMBAJI
nyota wa African pop, Tuface Innocent maarufu kama 2face Idibia na
mpenzi wake wa muda mrefu, Annie Macauley wamefunga ndoa ya kimila
mwishoni mwa wiki iliyopita na kuibua mjadala mzito baada ya kuzawadiwa
gari aina ya Prado Jeep na gavana wa Jimbo la Akwa Ibom, Dk. Godswill
Akpabio.
Mbali
na zawadi hiyo, gavana huyo pia ameahidi kugharamia wanafamilia 20 wa
Annie anayetoka katika jimbo hilo, ambao hawana uwezo wa kwenda Dubai
ambako wawili hao watafunga ndoa rasmi baadae mwezi huu
Kamishina
wa mawasiliano wa jimbo hilo, Aniekan Umana, alithibitisha Alhamisi
wiki hii kwamba gavana Akpabio ameamua kumsaidia Annie Idibia, hivyo
familia yake na marafiki wa karibu ambao ni raia wa Akwa Ibom wasioweza
kumudu gharama ya safari ya Dubai watakuwa pamoja nae kwenye sherehe
hizo.
Wakati
watu wakihoji sababu ya gavana huyo kuingia gharama kwa ajili ya harusi
hiyo, Umana alisema kwenye taarifa ya ofisi ya jimbo kuwa, wenza hao
wamefanikiwa kukusanya pamoja mastaa na watu kibao maarufu, jambo ambalo
ni zuri kwa uchumi wa jimbo lake.
“Harusi
ya Annie na Tuface kuletwa Akwa Ibom ni jambo zuri kwa uchumi wa jimbo,
na hili lisingeliweza kutokea hata kwa matangazo ya naira milioni 3,”
alisema Umana akirejea jumla ya fedha zinazotarajiwa kutumika kukata
tiketi kwa familia na rafiki wa Annie kutoka Dubai.
No comments:
Post a Comment