LONDON, ENGLAND
SAMIR
NASRI anakaribia kufikia mwisho wa maisha yake Manchester City na sasa
vimwaga wa Ufaransa, Paris St-Germain wanapiga hatua kutaka kumsajili.
Kiungo
huyo mwenye mkataba hadi mwaka 2015 amekuwa si chaguo la kwanza kwa
bosi Roberto Mancini na ameanzishwa karibu nusu tu ya mechi za City
katika Premier League msimu huu.
Mancini
hafurahishwi na kiwango cha staa huyo wa Ufaransa aliyenunuliwa kutoka
Arsenal kwa pauni milioni 24 mwaka 2011 na kuisaidia City kutwaa ubingwa
msimu uliopita.
Lakini
PSG walio vinara wa Ligue 1 ya Ufaransa wamefungua ukurasa wa
majadiliano na washauri wa kiungo huyo aliyezaliwa Marseille miaka 25
iliyopita.
No comments:
Post a Comment