EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, March 23, 2013

Hukumu ya Sheikh Ponda Aprili 18

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Aprili 18, mwaka huu inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (55) na wenzake 49.

Mbali na kupangwa kwa tarehe ya hukumu hiyo, Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa jana aliutaka upande wa mashtaka na utetezi kuwasilisha hoja zao kama washtakiwa hao watakuwa na hatia ama la, Aprili 3, mwaka huu.
Juzi wakati Sheikh Ponda akijitetea aliieleza mahakama hiyo, kuwa yeye hana nyaraka za umiliki wa Kiwanja cha Malkazi Chang’ombe bali historia ya eneo hilo inawafanya wao kuwa wamiliki.

Sheikh Ponda na wenzake hao 49, wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kuingia kwa jinai, kuvamia ardhi inayomilikiwa na Kampuni ya Agritanza Ltd kwa nia ya kujimilikisha isivyo halali, wizi wa mali yenye thamani ya Sh 59.6 milioni na uchochezi.

Akijitetea dhidi ya mashtaka hayo, Sheikh Ponda, akiongozwa na wakili wake, Juma Nassoro, alidai kuwa awali kiwanja hicho kilikuwa kinamilikiwa na Taasisi ya Jumuiya ya Kiislamu ya East African Muslim Welfare Society (EAMWS) ambayo ilivunjwa na Serikali mwaka 1958 na Serikali kuunda chombo kingine kilichosajiliwa kama Bakwata.
Alidai kuwa Bakwata iliundwa ili kusimamia shughuli zilizokuwa zikiendeshwa na Taasisi ya Jumuiya ya Kiislamu ya East African Muslim Welfare Society na siyo mali kama majengo, viwanja na hata shule.


“Tulitumia njia ya mazungumzo ya kidiplomasia kurejesha kiwanja cha Malkazi Chang’ombe kwa kuzingatia kuwa itatatua mgogoro huo katika njia nyepesi” alidai Sheikh Ponda.
Alidai Sheikh Ponda.Nyerere sasa tusilete mijadala isiyokuwepo.”
Hata hivyo, Sheikh Ponda alikubali kuwa yeye ni miongoni mwa watu waliohusika kutoa taarifa kwa maimamu wa misikiti mbalimbali kuwaeleza waumini wao kushiriki kujitolea katika ujenzi wa msikiti wa muda uliojenga katika eneo la Malkazi Chang’ombe Oktoba 11 na kukamilika Oktoba 14, mwaka jana.

Alidai kuwa walijenga msikiti huo baada ya kufanya makubaliano na mmoja wa wamiliki wa Kampuni ya Agritanza Ltd, Hafidhi, na kukubaliana kuweka alama ambayo kila Muislamu akiiona ataiheshimu na kutofanya shughuli zake binafsi katika eneo hilo na kupendekeza kujenga msikiti huo wa muda.
Kuhusu kukamatwa kwake

Sheikh Ponda alidai kuwa yeye alikamatwa Oktoba 16, 2012, nyakati za saa 4 kasoro usiku alipokuwa akijiandaa kuingia katika Msikiti wa Tungi Temeke , akipanda ngazi alitokea mtu mmoja aliyekuwa kwenye gari nyeusi aina ya Toyota Harrier akimtaka amfuate.Alidai kuwa na yeye pia alimshauri pia amfuate na baadaye alimua kuachana naye na kuingia ndani ya msikiti huyo, lakini alisikia kishindo cha gari na alipogeuka nyumba aliona gari tatu deffender zilizojaa askari wa FFU wakiwa wamebeba silaha. 
CHANZO MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate