Mashabiki wa klabu ya Simba jana walizichapa wenyewe kwa wenyewe
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
wakati walipokuwa wakimsubiri Mwe-nyekiti wao, Ismail Aden Rage
aliyekuwa akitokea nchini India kutibiwa.
Mashabiki hao wa Simba wal-izichapa baada ya
kugundua baadhi yao walikwenda uwan-jani hapo kwa lengo la kum-fanyia
vurugu mwenyekiti wao wakati wa mapokezi hayo.
Gazeti hili lilishuhudia mashabiki hao wa Simba
walio-kaa kwa muda wa saa mbili uwanjani hapo kabla ya kuwasi-li kwa
Rage na pia lilishuhudia mashabiki hao wakitwangana.
Kabla ya mashabiki hao kut-wangana, mashabiki
waliokuwa wakimuunga mkono mwenyekiti wao walikuwa wakiimba nyimbo
mbalimbali na walionekana wenye matumaini makubwa na Rage huku
wakisisitiza bado wanautambua uongozi wake na hakuna anayeweza kumuondoa
zaidi yao wenyewe.
Hata hivyo, baadaye lilitokea kundi dogo la
mashabiki wa Simba ambalo lilisadikiwa kuwa ni kundi la Mpira Pesa
ambalo limekwenda uwanjani hapo kwa ajili ya kufanya fujo na hivyo
kuanza kushambuliwa kwa makonde wakidaiwa kuhusika na mkutano
uliotangaza kum-wondoa Rage madarakani.
Mmoja wa mashabiki wa kla-bu hiyo ambaye
alijitambulisha kwa jina la Shaban anayetokea tawi la makao makuu ya
klabu ya Simba alisema bado Rage ataendelea kuwa Mwenyekiti na
hawayatambui mapinduzi yali-yofanywa na baadhi ya watu wa Simba.
“Yale yalikuwa maneno ya watu, sisi hapa ndiyo
Simba, bila sisi hakuna Simba, Rage ndiyo Mwenyekiti wetu na ataendelea
kukaa madarakani mpaka sisi tutake wenyewe kumwondoa, wale Mpira Pesa
walikuwa wan-ajisumbua na hapa hang’olewi mtu, hii ndiyo Simba bwana na
sisi ndiyo wenye timu,” alisema Shaban huku wenzake wakimuunga mkono kwa
kupiga mavuvuzela.
Mara baada ya Rage kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere, alipitia mlango wa watu maalumu VIP na ali-potoka aliwasalimia
mashabiki waliokuwa wakimshangilia na alikwenda moja kwa moja kati-ka
gari aliloandaliwa huku aki-waambia waandishi wa habari wajionee wenyewe
kama kuna mapinduzi yoyote yanayozung-umzwa juu yake.
“Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwa
kuende-lea kupigania afya yangu kwani kwa sasa ni ninaendelea vizuri,
wingi wa watu hawa unatosha kunitambua mimi ni Mwenyeki-ti halali wa
Simba na ninashan-gazwa kusikia kuna mapinduzi, hii ni ajabu
sana,”alisema Rage.
Alisema,”Nyinyi wenyewe ni mashuhuda, angalieni
hapa kuna mapinduzi kweli? wanao-taka mapinduzi ni watu wach-ache
wanaotaka kuiharibu Sim-ba na kuleta migogoro isiyofaa?, sijiuzulu hata
kidogo eti kwa kuwaogopa matapeli wachache, nitafanya hivyo endapo
nitaona mimi mwenyewe napaswa kuji-uzulu, lakini siyo kwa
kushini-kizwa.”
No comments:
Post a Comment