NI
kama maji yamefuata mkondo, anatesa sana kwenye filamu za kibongo
hususan linapokuja suala la kushika camera, huyo ni Kabuti Onyango.
Baba yake nae anatesa kwenye filamu za kibongo hasa linapokuja suala la kuvunja mbavu za watu, huyo ni Issa Joseph “Onyango”.
Unapozungumzia wapiga picha bora wa filamu za kibongo, lazima umtaje Kabuti.
Kwa mwaka huu anaongoza kwa mbali kwa kushuti filamu zilizokimbiza sokoni huku zikiwa zimeshiba ubora wa picha.
Hapa ni Kabuti (kushoto) na Kingwengu
Kabuti anaimbia Saluti5 kuwa alianzia kwenye kuigiza jambo ambalo kwa sasa linamsaidia sana kwenye upande wa camera.
“Ukiwa
umeshiriki uigizaji halafu ukahamia kwenye camera kila kitu kinakuwa ni
mteremko, unakuwa ni mtu unayejua mahitaji ya pande zote mbili” anasema
Kabuti mzaliwa wa Dar es Salaam aliyepata elimu yake ya sekondari
katika shule ya Tegeta.
Miongoni mwa filamu nyingi alizopiga ni pamoja na Pusi na Paku, Hekima, Majanga na Chocolate.
Onyango baba mzazi wa Kabuti
Uwezo
wa Kabuti Onyango aliyefanya kazi karibu na wasanii wote wakubwa,
unatagemewa kuonekana tena kwenye filamu mpya ya Nisha “Tikisa”
inayotarajiwa kutoka baadae mwaka huu.
Nini
siri ya mafanikio yake? Kabuti anasema ni kuipenda kazi yake, kuheshimu
mikataba ya wateja wake, kuzingatia miiko ya kazi, ari ya kujifunza,
kutokuwa na tama ndiyo siri ya mafanikio aliyonayo hivi sasa.Habari na www.saluti5.com
No comments:
Post a Comment