Maneno haya manne yenye nguvu ya kumdatisha mwanamke, ambayo ni NAKUPENDA, NAKUHITAJI, SAMAHANI na ASANTE.
Ni
wazi kwamba kuna wanaume wengi ambao huanza na gia kubwa ya maneno hao
wamebainika kupoteza mvuto wa kimapenzi waliokuwa nao mwanzo kwa wapenzi
wao. Binafsi nathibitisha hili kwa kuwa nimeshafanya uchunguzi kupitia
wanaume wanaonijia kutaka majibu ya kwa nini wapenzi wao wamewageuka na
kutokuwapenda kama awali.
Kabla ya kuwashauri nimekuwa nawadodosa na hatimaye kutambua kuwa waliacha kutumia maneno hayo mara tu walipoona wamefanikiwa walichokuwa wanakitafuta.
Kabla ya kuwashauri nimekuwa nawadodosa na hatimaye kutambua kuwa waliacha kutumia maneno hayo mara tu walipoona wamefanikiwa walichokuwa wanakitafuta.
Kama nilivyosema
neno la kwanza lenye nguvu ya kumteka kimapenzi mwanamke ni NAKUPENDA.
Neno hili ni tiba inayoponya hofu na kumfanya mwanamke ajiamini.
Neno
la pili, NAKUHITAJI. Kama inavyokuwa wakati wa kutongoza, mwanamke
anapenda kuambiwa neno hilo na kufanyiwa vitendo vinavyoonesha
kuhitajika kwake katika maamuzi, matembezi, faraja na muongozo wa
kimaisha. Sambamba na hilo mwanamke anapenda sana kupewa ASANTE katika
yale anayofanya.
Jambo la mwisho kabisa ni SAMAHANI. Ndugu zangu
kuna wanaume ambao hawako tayari kuomba msamaha kabisa hata kama
wamekosa kosa kubwa na la wazi kiasi gani? Kifupi tabia hiyo haipendezi.
Ni busara kwa mwanaume kumuomba radhi mpenzi wake, ili naye ajione ni
mwenye mamlaka na hivyo kuzidisha upendo na uangalizi wa tabia mbaya za
mwanaume.
No comments:
Post a Comment