Na. Mwandishi Wetu
MPIGAPICHA wa kujitegemea ambaye ni mlemavu wa miguu wa mjini hapa, Elias Ngole Ngoswe amemwangukia msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu kwa kumuomba msaada ili aweze kutibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandishi wetu Jumanne
iliyopita, Ngoswe ambaye ulemavu wake ulitokana na kugongwa na gari
kwenye mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya
Sekondari ya Wasichana Korogwe, Februari 2, mwaka jana na akavunjika
miguu na mfupa wa nyonga, alisema uamuzi wake wa kumuomba msaada Wema
unatokana na kuvutiwa kwake na msaada aliompa msanii mwenzake, Kajala
Masanja ambaye alimuokoa kufungwa jela kwa kumtolea faini.
“Nimegundua
kuwa Wema ana huruma sana nami nikaamua nimuombe msaada kupitia gazeti
hili kwani nina matatizo mazito. Nilipovunjika miguu na nyonga
nilikimbizwa Hospitali ya Wilaya Magunga, Korogwe baadaye nikahamishiwa
Hospitali ya Tumbi Kibaha, nikalazwa miezi mitatu baadaye nilihamishiwa
Muhimbili ambako bei niliyoandikiwa nilipe imenishinda,” alisema Ngoswe.
Kwa
mujibu wa hati ya malipo ya Muhimbili ya Septemba 10 mwaka jana (nakala
tunayo), Ngoswe alitakiwa alipe gharama za matibabu shilingi 9,798,250
ambazo hana.
“Ni fedha nyingi sana ambazo kutokana na ugumu wa maisha, nimeshindwa kulipia. Namuomba Wema na watu wengine wenye huruma wanisaidie ili nitibiwe,” alisema kwa masikitiko Ngoswe. Wema au yeyote aliyeguswa na habari hii awasiliane naye kwa namba 0766 224 284 na Mungu atawabari

MAJINA YA WATU YANATAFSRI VITENDO VYAO, JINA LA WEMA NAONA LINATAFSIRI HALISI, WAPO WALIOPEWA MAJINA YA CHUKI,SHIDA NA MATATIZO, MAJUTO NK AMBAO YAMEONEKANA KUFANANA NA MAISHA YAO HALISI, TUCHAGUE MAJINA MAZURI, WEMA MUNGU AENDELEE KUKUTIA MOYO HUO WA WEMA NA HURUMA
ReplyDelete