MTOTO Debora Riziki (3), mkazi wa Kijiji cha Isange wilayani Rungwe, ameuawa na mwili wake kuzikwa sebuleni katika nyumba yao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, alisema jana kuwa
tukio hilo lilitokea juzi majira ya 7:40 mchana na anayetuhumiwa
kuhusika na mauaji hayo ni baba mzazi wa mtoto huyo, Riziki Mwangoka
(27).
Alisema sababu ya kufanya ukatili huo ni kutokana na mgogoro wa kindoa
kati ya baba huyo na mama wa mtoto huyo, Esther Msafiri Mwambenja (23),
mkazi wa Kijiji cha Kimbukwe.
Kamanda Diwani alisema kutokana na mgogoro wa muda mrefu wanandoa hao
walitengana na kwamba siku ya tukio baba huyo alifika nyumbani kwa mzazi
mwenzake na kumchukua mtoto huyo kwa nguvu na kwenda kumuua.
Alisema mwili wa marehemu umeshafanyiwa uchunguzi na umekabidhiwa kwa
ndugu kwa ajili ya mazishi. Polisi wanaendeea na utaratibu kwa ajili ya
kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.
Kamanda Diwani alitoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi ili kuepusha matatizo yanayoweza kuepukika.
No comments:
Post a Comment