Ghorofa la hoteli inayosadikiwa kutokea tukio hilo.
Mwanamke
mmoja raia wa Uingereza anaendelea kupata nafuu kufuatia majeraha
aliyoyapata baada ya kuruka kupitia dirishani katika hoteli aliyokuwemo,
kukimbia kile kilichoitwa shambulio la kutaka kubaka katika mji wa Agra
nchini India.
Kwa mujibu wa Polisi, tukio hilo limetokea katika eneo la Cantonment mjini humo, katika majira ya alfajiri.
Naibu
Supaintendent wa Polisi Simranjit Kaur amekaririwa akisema kuwa
mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 31, aliruka kutoka katika dirisha la
ghorofa ya pili baada ya mmiliki wa hoteli hiyo kujaribu kuingia
chumbani kwake akidai kutaka kuchuliwa misuli (Massage).
Amesema mwanamke huyo aliingiwa na uoga wa kubakwa uliosababisha kuruka ghorofani humo.
Hata
hivyo Kaur amesema polisi inamshikilia mmiliki wa hoteli hiyo na huenda
wakafungia leseni ya biashara hiyo, kutokana na matokeo
yatakayopatikana baada ya uchunguzi kukamilika.
No comments:
Post a Comment