Mabao matatu ya nyota wa TP Mazembe ya DR Congo, Mbwana Samata
na Thomas Ulimwengu yalitosha kuipa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa
Stars’ ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Morocco katika mechi ya
kutafuta tik-eti ya kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia, Brazil
2014.
Kwa ushindi huo, Stars sasa imefikisha pointi sita
na hivyo kuendelea kushika nafasi ya pili katika Kundi C ikiwa nyuma ya
Ivory Coast yenye pointi saba, baada ya kuifunga Gambia mabao 3-0 juzi.
Mshambuliaji Ulimwengu aliyeingia akitokea benchi
kipindi cha pili alifunga bao la kwanza la Stars dakika ya 46, kabla ya
kumtengenezea nyota mwenzake wa TP Mazembe, Samata aliyefunga men-gine
mawili dakika ya 66 na 80.
Stars ilianza mchezo huo kwa kasi na kulifikia
lango la wapinzani wao dakika ya pili tu ya mchezo wakati shuti la
kiungo Amri Kiemba ilipogonga mtambaa wa panya kabla ya mabeki wa
Morocco kuon-doa mpira kwenye hatari.
Dakika ya tisa Morocco ilijibu mapi-go na kona
iliyochongwa na Barrada Abdellaziz ilimfikia Abuurazouk Hamza ambaye
alipiga kichwa kilichotoka senti-mita chache kwenye lango la Stars.
Baada ya kashikashi hizo, kila upande ulijaribu
kutuliza mpira chini na kupelekeana mashambulizi kwa zamu. Hata hivyo
hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika hakuna timu ili-yokuwa
imetingisha nyavu.
Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kuz-induka upya na kupeleka
mashambulizi kuelekea kwa wapinzani wao Morocco na kupata bao dakika
moja tu kupitia kwa Ulimwengu, ambaye ulikuwa ni mpira wake wa kwanza
kuugusa.
Ulimwengu aliyeingia uwanjani kipindi cha pili
akichukua nafasi ya Mwinyi Kazi-moto alipachika bao hilo kwa shuti kali
la karibu lililomshinda kipa wa Morocco, Lamyaghir Nadir kutokana makosa
ya mabeki wake waliochelewa kuondosha mpira kwenye eneo lao la hatari.
Samata ambaye takriban muda wote wa mchezo alikuwa
kero kwa mabeki wa Morocco alifunga bao lake la kwanza kwa shuti la
pembeni baada ya kuwa-toka mabeki wa Morocco kisha kufunga lingine kwa
kumalizia pande la kukata la Ulimwengu.
Dakika ya 81, mwamuzi wa mchezo huo Helder Martins
kutoka Angola alim-wonyesha kadi nyekundu Achachakir Abdelkarim wa
Morocco baada ya kum-tolea lugha chafu na kumsukuma aki-dai alitendewa
faulo na Ulimwengu kabla hajatoa pasi ya bao kwa Samata.
Katika mechi hiyo, kocha wa Taifa Stars, Kim
Poulsen alifanya mabadiliko dakika ya 64, kwa kumtoa Ngasa nanafasi yake
kuchukuliwa na Athumani Iddi, pia dakika ya 89 alimtoa Samata na
kum-wingiza John Bocco.
Dakika ya 90, Chaeni Kamal alifunga bao la
kufuatia machozi kwa upande wa Morocco na hivyo kufanya matokeo kuwa
3-1. Akizungumza baada ya mechi kumal-izika, kocha Kim alisema:
“Nimefurahish-wa na ushindi huu, vijana wangu waliji-tuma na wanastahili
ushindi, ninaomba Watanzania waendelee kuiunga mkono Taifa Stars.”Alisema: “Kipindi cha kwanza Moroc-co walikuwa wakijilinda na kufanya
mashambulizi ya kushtukiza huku wakitegemea pia mipira iliyokufa.”
No comments:
Post a Comment