UKARABATI wa wodi namba sita katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro uliofanywa na Benki ya CRDB umegharimu sh milioni 50.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema jana
kuwa fedha zilizotumika kufanya ukarabati huo ni kutoka katika akaunti
ya watoto ya Junior Jumbo iliyopo katika benki hiyo na kwamba iliamua
kufanya ukarabati huo baada ya kuona ubovu wa wodi hiyo.
Alisema benki hiyo imekuwa na vipaumbele vyake katika kuchangia
masuala mbalimbali ya kijamii hasa katika masuala ya afya, elimu na
mazingira.
“CRDB imekuwa ikilipa kodi kubwa, tena bila kuchakachua na kila
mwaka tumekuwa tukilipa sh bilioni moja, jambo ambalo tunajivunia,”
alisema Dk. Kimei.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashidi, akizindua
wodi hiyo aliipongeza CRDB kwa uamuzi wa kuifanyia ukarabati wodi hiyo
na kuyataka mashirika na taasisi nyingine kuiga mfano huo ili kuboresha
huduma za afya kwa wananchi.
Pia aliwataka wananchi hasa watumiaji wa wodi hiyo kutunza miundombinu iliyopo ikiwa ni pamoja na vifaa.
No comments:
Post a Comment