Mapigano mapya yaliyozuka kati ya askari usalama wa Nigeria na
kundi la wanamgambo wa Boko Haram huko katika kijiji cha Jashwa
kilichopo katika jimbo la Yobe kaskazini mashariki mwa nchi hiyo,
yamepelekea kuuawa watu wasiopungua 25.
Mkuu wa polisi katika jimbo la Yobe Alhaji Sanusi Rufai amesema kuwa,
kati ya watu hao waliouawa ni pamoja na wanamgambo 20 wa Boko Haram na
askari 5 na kwamba, askari wengine wawali wamejeruhiwa na kulazwa
hospitali. Sanusi amesema kuwa, wanamgambo hao walivamia nyumba ya
kiongozi wa benki moja iliyopo jimboni hapo na kuiba pesa zote
zilizokuwemo.
Wakati huo huo, msemaji wa polisi ya Nigeria amesema kuwa, katika
mapigano hayo askari usalama wa nchi hiyo wamefanikiwa kudhibiti aina
mbalimbali za silaha na mabomu ya kurusha kwa mkono na magari matatu
vilivyokuwa vikidhibitiwa na wanamgambo hao.
No comments:
Post a Comment