Mkinga. Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mboni Mgaza amewataka wanawake wa
Mkinga kuunda vikundi vya ushirika, ili kuweza kujikwamua na maisha
pamoja na kuimarisha biashara zao na kuacha kukaa nyumbani.
Akizungumza
katika mafunzo na wanachama wa Vikoba wa Maramba na kufadhiliwa na
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Mgaza alisema siri ya kutoka
katika dimbwi la umaskini ni kujishughulisha na kazi za ujasiriamali.
Alisema wilaya hiyo yenye mwambao wa bahari pamoja na ardhi nzuri ya
kilimo cha mbogamboga na matunda ni fursa tosha kwa wajasiriamali wa
kike na kiume kubuni mbinu mbadala za kujikwamua na umaskini.
Alisema
kutokana na ufunguzi wa barabara mpya ya kiwango cha Lami Tanga,
Horohoro, ni wakati wa wafanyabiashara wakubwa na wajasiriamali kutafuta
masoko ya bidhaa zao katika masoko yaliyoko ndani ya Jumuiya ya Afrika
ya Mashariki. Akizungumza katika mafunzo hayo, Mshauri Elekezi wa
Masuala ya Ujasiriamali TPSF, Jane Gonsalves,alisema sekta hiyo ilifanya
uchunguzi katika wilaya hiyo na kugundua wajasiriamali hawana elimu ya
biashara (Salim Mohammed)
No comments:
Post a Comment