Ile
filamu ya Love & Power ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na
wapenzi wengi wa filamu hatimaye leo Ijumaa
tarehe 12th April 2013 itazinduliwa na kuingia sokoni rasmi na
kusambazwa nchi nzima na kampuni ya mahiri ya usambazaji wa filamu ya
Steps Entertainment Ltd.

Filamu ya Love & Power Bwana
Myovela Mfwaisa amesema kuwa “Filamu ya Love & Power ni filamu ya
mwisho kutengenezwa na marehemu The Great Kanumba inaingia sokoni na
kuwafikia watanzania wote siku ya ijumaa,”
Hivyo basi hii itakuwa fursa pekee kwa wa tasnia ya filamu na
watanzania wote kwa ujumla na kuweza kujionea kazi bora iliyotengenezwa
na gwiji la filamu na balozi aliyetangaza tasnia ya filamu ya Tanzania
nje ya mipaka ya Tanzania, kila mpenzi wa filamu aweke ahadi kutokuikosa
filamu bora na ya mwisho kuigizwa na marehemu nyota wa filamu Tanzania.
Filamu ya Love & Power Bwana Myovela, “Filamu ya
Love & Power imetengenezwa na kampuni ya Kanumba the Great film kwa
kushirikia na Steps Entertainment Ltd ikiwa imeandikwa na Ally Yakuti,
Filamu ya Love & Power imeshirikisha wasanii nyota katika tasnia ya
Filamu Tanzania kama Hussein Mkiety ‘Sharomilionea’, Irene Paul, Patcho
Mwamba, Grace Mapunda, Hartman, Rammy Galis pamoja Seth Bosco ambaye ni
mdogo wake na marehemu kuongozwa na Steven Kanumba, Watayarishaji wakuu
ni Steps Entertainment Ltd imetengenezwa hapa jijini Dar es Salaam
katika maeneo tofauti tofauti.
Lugha
iliyotumika katika filamu hiyo ni Kiswahili lakini pia Lugha ya
kiingereza imetumika kama ‘Subtitles’. Umri wa kutazama filamu ya Love
& Power ni miaka 16 ni filamu nzuri inayotazamwa na watoto pamoja na
familia, iliyopewa kibali cha ukaguzi Kutoka Bodi ya ukaguzi wa filamu
na michezo ya kuigiza Tanzania.
Katika kuhakikisha kuwa wasanii wanafaidika na kazi zao tunaomba kila
mdau wa filamu awe mlinzi wa kazi hizi za filamu za kitanzania kwa
kupambana na Maharamia wa kazi za Wasanii wa filamu, pia tunawaomba
wapenzi wa filamu kununua nakala halali yenye nembo ya Steps
Entertainment Ltd, hiyo itachochea maslahi kwa wasanii wa Tanzania na
kuongeza ajira kwa vijana ili kufikia hilo nunua filamu ya Love &
Power halali.
Unaweza kupata filamu ya Love & Power kwa kuwasiliana na Wasambazaji kwa namba hizi: 0716 788 805, 0713 570 581
Asanteni.

Marehemu Kanumba akiwa katika moja ya filamu yake enzi za uhai wake.
Unaweza kupata filamu ya Love & Power kwa kuwasiliana na Wasambazaji kwa namba hizi: 0716 788 805, 0713 570 581
Asanteni.
No comments:
Post a Comment