BONGE la Bwana ndio jina linalovuma kwa msanii wa filamu Bongo Jacob
Stephen ‘JB’ kwa sasa Jb ameingia rasmi katika ujasiriamali baada
kuzindua mavazi yake ya JB Wear na kuwauzia wapenzi wa filamu wanaopenda
kumuunga mkono katika harakati zake za filamu Bongo, JB anasema kuwa
naye anaungana na wasanii wakubwa Duniani ambao pamoja na kazi za Sanaa
pia umiliki biashara nyingine.
“Nafahamu kuwa kwa sasa jina langu katika sanaa limekuwa zaidi na
ninahitaji kuwa na lebo yangu kwa ajili ya watu wangu ambao kila siku
wananunua kazi zangu baada ya kupokea maoni nimeamua kutangaza mavazi
yangu JB Wear na JB Bonge la Bwana tayari T-Shirt na Top zimeingia na
zinapatikana katika maduka mbalimbali,”anasema JB.
JB anakuwa msanii wa kwanza wa filamu kuuza nguo zenye alama yake
baada kuona wasanii wa kizazi kipya Bongo fleva wakiwa na nguo zao kama
vile AY na Gangwe Mob waliwahi kufanya hivyo, JB anatamba na filamu kali
kama Senior Bachelor, Nakwenda kwa Mwanangu, Regina na filamu
nyinginezo zilimpa uigizaji bora katika filamu.
T-shirt hizo kwa sasa zinagombewa na nyota wa filamu kibao kulingana
na ubora wake zilivyotengenezwa na kuvutia mbunifu wa kazi hiyo
ameonekana kuwa makini katika ubunifu wake, kwa wale ambao hawawezi
kufika katika maduka zinakopatikana JB Wear wanaweza kuwasiliana na
wauzaji kwa namba .0713 37 21 94….0766 50 45 60 na utapata mzigo ulipo
USIKOSE BONGE LA BWANA.
No comments:
Post a Comment