“MIMI
nipo katika kundi la watu ambao hawaelewi mapenzi.” Hiyo ni kauli ya
staa wa muziki wa Pop wa Marekani, Rihanna akiwaambia mashabiki wake.
Rihanna
alitoa kauli hiyo akiwa kwenye steji huko Los Angeles usiku wa Jumatatu
iliyopita, akithibitisha uvumi kwamba ameachana tena na mpenzi wake
Chris Brown.
Akihutubia
umati wa watu katika shoo yake iliyopigwa ndani ya Staples Center,
aliuliza: "Ni wangapi kati yenu wapo kwenye mapenzi? Wangapi kati yenu
mnachukia mapenzi?
"Wangapi kati yenu hawaelewi mapenzi? Mimi niko katika kundi hilo. "
Rihanna alitoa nafasi ya pili kwa mwimbaji Brown baada ya kumpa kichapo kikali mwaka 2009.
Brown
alihukumiwa ‘kifungo cha nje’ miaka mitano, huku akitakiwa kufanya kazi
za jamii kwa saa 1,400 kutokana na kitendo chake hicho.
Hata hivyo, nyota hao walizika tofauti zao na kutangaza kurudiana mwezi Februari mwaka huu.
Via www.saluti5.com
No comments:
Post a Comment