MEYA wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, amesema halmashauri hiyo
haihusiki na tukio la kuanguka kwa jengo la ghorofa 16 lilitokea wiki
iliyopita na kuua zaidi ya watu 30. Akizungumza kwenye kikao cha dharura
cha Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo jana, alisema halmashauri hiyo
haina mamlaka ya usimamizi wa masuala ya ujenzi.
“Kutokana na taratibu zilizokuwa zimezoeleka tangu huko nyuma usimamizi wa shughuli za ujenzi mjini zimeonekana kuwa mamlaka ya usimamizi ni halmashauri ya mji, manispaa au jiji husika na siyo wadau wengine.
“Kwa ujumla dhana hii siyo sahihi hata kidogo. Wadau katika sekta hii ni wengi ambao wanapaswa kusimamia shughuli zote za ujenzi pamoja na ubora wa kazi zinazofanywa na wakandarasi, wataalamu washauri kwa maana ya wahandisi na wasanifu majengo,” alisema.
Hadi sasa watu tisa wamekwisha kukamatwa kuhusuaiana na tukio la kuanguka jengo hilo, wengi wao wakiwa ni maofisa wa Halmashauri ya Wilaya ya |Ilala. Hao ni Mhandisi Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Ogare Sallu,Mhandisi wa Majengo, Godluck Mganga, Mkaguzi wa Majengo Wilbrod Mulyagusu na Vedasto Ferdnand ambaye ni Mchambuzi wa Ubora na Gharama za Ujenzi.
Silaa alisema kazi kubwa ya halmashauri ni kufuatilia kama muombaji anajenga kama alivyoomba katika mchoro iliyopitishwa.
“Kwa mantiki hiyo halmashauri haina mamlaka ya kusimamia majengo makubwa iwe ya umma au ya binafsi,” alisema Silaa.
Silaa
alisema mujibu wa sheria, kuna taasisi mbalimbali zinazohusika ambazo
ndizo zimekabidhiwa mamlaka ya kusimamia shughuli zote zinazohusiana na
masuala ya ujenzi.“Kutokana na taratibu zilizokuwa zimezoeleka tangu huko nyuma usimamizi wa shughuli za ujenzi mjini zimeonekana kuwa mamlaka ya usimamizi ni halmashauri ya mji, manispaa au jiji husika na siyo wadau wengine.
“Kwa ujumla dhana hii siyo sahihi hata kidogo. Wadau katika sekta hii ni wengi ambao wanapaswa kusimamia shughuli zote za ujenzi pamoja na ubora wa kazi zinazofanywa na wakandarasi, wataalamu washauri kwa maana ya wahandisi na wasanifu majengo,” alisema.
Hadi sasa watu tisa wamekwisha kukamatwa kuhusuaiana na tukio la kuanguka jengo hilo, wengi wao wakiwa ni maofisa wa Halmashauri ya Wilaya ya |Ilala. Hao ni Mhandisi Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Ogare Sallu,Mhandisi wa Majengo, Godluck Mganga, Mkaguzi wa Majengo Wilbrod Mulyagusu na Vedasto Ferdnand ambaye ni Mchambuzi wa Ubora na Gharama za Ujenzi.
Silaa alisema kazi kubwa ya halmashauri ni kufuatilia kama muombaji anajenga kama alivyoomba katika mchoro iliyopitishwa.
“Kwa mantiki hiyo halmashauri haina mamlaka ya kusimamia majengo makubwa iwe ya umma au ya binafsi,” alisema Silaa.
Alizitaja baadhi ya taasisi hizo kuwa ni Bodi ya Wasanifu Majengo ambayo ilipewa majukumu ya kusimamia shughuli na utendaji kazi wa wasanifu majengo, kukagua shughuli zote za ujenzi na kuhakikisha kuwa kazi ya ujenzi inafanywa na mtu aliyesajiliwa.
“Bodi ya Usajili wa Wahandisi ambayo ina kazi ya kufuatilia na kusimamia shughuli na utendaji kazi wa wahandisi ikiwa ni pamoja na kampuni zinazofanya kazi ya utaalamu, na Bodi ya Wakandarasi (CRB) ambayo inasimamia usalama mahali pa kazi na kusimamia miradi ya ujenzi kwa kutoa kibali na kusajili,”alisema Silaa.
No comments:
Post a Comment