Mtu huyo
aliyetambuliwa kwa jina la Jerome Onesmo (53) amekutwa amekufa kandokando ya
barabara iendayo mgodi wa uchimbaji madini ya Nickel kata ya Bugarama wilaya ya
Ngara mkoani Kagera.
Afisa
mtendaji wa kijiji cha Rwinyana kata ya Bugarama wilayani Ngara Bw Venace John
amesema mtu huyo aliondoka nyumbani kwake April 6 saa 11 jioni kwenda
kusaga mahindi na alikutwa njiani kesho yake akiwa amefariki dunia.
Akizungumza
na wanahabari mtoto wa pili wa marehemu Nuwaka Pambano (32) alisema baba yake
alikuwa amekunywa pombe kupita kiasi na alipokuwa njiani kwenda kusaga ambapo alikuwa
akianguka hovyo na alipowekwa kando kando ya barabara aliahidi kunyanyuka na hadi pale alipokutwa
amepoteza maisha.
Aidha mtoto
mkubwa wa marehemu Sibomana Jerome 35 akiwa katika eneo la tukio alikokutwa
baba yake akiwa amefariki dunia , aliwashangaza wananchi waliofika kushuhudia
mwili wa marehemu pembeni mwa barabara kwa kujivua nguo na kujitosa kwenye madimbwi ya maji machafu.
Kijana huyo
aliwatuhumu wananchi kuwa baba yake amefariki kwa kupewa sumu na ndugu zake
wanaogombania mashamba yanayotarajiwa kutolewa fidia na mradi wa uchimbaji
madini aina ya Nickel kijiji humo.
Kamanda wa
jeshi la polisi mkoani Kagera Philipo Karangi amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kwamba jeshi la polisi wilayani Ngara linafanya uchunguzi kujua chanzo
cha kifo cha mwananchi huyo.
|
No comments:
Post a Comment