Ama
hakika duniani kuna mambo! Na lisemwalo lipo kama halipo basi laja. Ni jambo ambalo ni vigumu kuliamini lakini
ukweli wa mambo ni kwamba limetokea mjini Kahama, Mkoa wa Shinyanga, kiasi cha kuleta mtafaruku kwa jamii.
![]() |
|
Mwajuma
akiwa
anapelekwa
kwenye gari
la
polisi bila kuachia
alichodai
ni "hazina"
ya
kazi yao.
|
Ni baada ya vikongwe viwili vinavyosadikiwa ni
vichawi kunusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali kufuatia kudondoka
kutoka angani.
Tukio hili la aina yake ambalo mbali na
kustaajabisha limeleta hofu kwa baadhi ya wakazi mjini Kahama, lilitokea usiku
wa kuamkia Aprili 3 mwaka huu katikati ya Kata za Majengo na Mhongolo zilizo
katika Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Vikongwe
hivyo vilikutwa vikiwa taabani huku vikiwa vimetapakaa kinyesi.
Vikongwe
hivyo, Mwajuma Samaka Mponi (70) mkazi wa kijiji cha Nduku katika Kata ya
Kinaga na Shija Nkwabi (80) mkazi wa kijiji cha Nyashimbi pia mkazi wa Kata ya
Mhongolo katika Halmashauri ya Mji wa Kahama, vilikumbwa na dhoruba la
kudondoka baada ya kugongana na wanga wenzao wengine watatu waliokuwa katika
shughuli zao angani.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mhongolo, Emmanuel
Kalolo, anasimulia kuwa vikongwe hivyo
vilionekana vikiwa hoi havijitambui vikiwa vimelala ambapo kimoja kilikuwa eneo
la Kindi’s Bar katika barabara ya kwenda Mhongolo huku mwingine akiwa mtaa wa
Bariadi karibu na Café Latino.
![]() |
|
Vikongwe
'sangoma'
Mwajuma
(kushoto)
na
Shija, wakiwa ndani
ya karandinga la polisi.
|
Kalolo
alisema kuwa Waendesha bodaboda (pikipiki) walianza kumshuhudia kikongwe
Mwajuma Mponi tangu alfajiri lakini hawakumjali kwa kudhani kuwa huenda ni
mlevi ama mwendawazimu.
Hali
iliendelea hivyo hadi alipotokea mtu mmoja ambaye aliingiwa na mashaka baada ya kumwona akiwa uchi wa mnyama tena
akiwa ametapakaa kinyesi.
Msamaria huyo, Kulwa Samson, kwa jina maarufu’ KR’ ambaye ni Meneja wa Café Latino, baada ya kumuona bibi huyo aliamua kumpatia msaada kwa kumuombea nguo katika nyumba za jirani.
Samson alisema alibaini hilo wakati kienda
Mhongolo kufuatilia kreti za bia. Baada ya kumsaidia, bibi huyo alimweleza kuwa
kuna mwenzake mtaa wa pili.
Walipomfuatilia walimkuta akiwa amezingirwa na watu waliokuwa
wamemshangaa.
Baada
pia ya kumsitiri alimchukua hadi kwa mwenzake na kuwafanyia mpango wa chakula.
Baada ya huduma hiyo aliwakabidhi kwa Kamanda
wa Wanawake Kata ya Majengo, Kuluthum Bujiku, ambapo walianza kuwasaili chanzo
cha kuwa katika madhia hayo.
Nao
bila kupepesa macho, vikongwe hivyo vilidai vilidondoka vikiwa katika shughuli
zao za kawaida za kila siku usiku.
Mashuhuda hao walisema kuwa vikongwe hivyo
vilidai vilikuwa vikitoka katika makao yao ya shughuli zao huko Nduku wakiwa na
wenzao watano wakielekea Dodoma kuhitimisha kilele cha sherehe za Pasaka.
Walisema
wakiwa angani walipata ajali ya kugongana na wenzao waliokuwa wakitoka eneo
jingine hivyo wakajikuta wamedondoka ardhini.
Vikongwe
hao vilieleza kuwa safari yao ya Dodoma ilikuwa ya kwenda na kurudi usiku
huohuo mara baada ya kukamilika kwa tafrija yao hiyo ya Pasaka.
Kwa
bahati mbaya, walidai, wakiwa njiani
kuelekea Dodoma walikumbwa na dhoruba hiyo na kudai baada ya kugongwa
“pikipiki” yao iliishiwa mafuta.
Walisema
kuwa wenzao watatu ambao waliishawahi kukumbwa na dhoruba hiyo mara nyingi,
walitoweka katika mazingira ya kutatanisha na kuwaacha wao wakitapatapa.
Waliongeza
kwamba shughuli hiyo ya usangoma
imewafikisha maeneo mbalimbali hapa nchini
na walikuwa hawajawahi kudondoka.
Baada ya maelezo hayo ambayo waliyatoa huku
kukiwa na umati wa watu ambao walitaharuki na kutaka kuwashushia kipigo,
sangoma hao walinusurika baada ya Samson kuwa tayari amewapigia simu polisi
ambao hawakufanya ajizi kufika eneo la tukio na kuwakuta watu wenye hasira
wakiwa wamejipanga kuwatoa uhai vikongwe hao.
![]() |
|
Vikongwe
'sangoma'
Mwajuma
(kushoto)
na
Shija, wakiwa ndani
ya karandinga la polisi.
|
Watu hao walipandishwa katika karandinga huku
kikongwe Mwajuma akigoma kuachia kifuko cheusi alichokuwa amekishika mkono wa
kulia ambacho alidai ni hazina yao muhimu.
Vilevile,
gari la oolisi lilipata wakati mgumu
kuondoka hapo kwani lilionekana kama vile gurudumu zake zinataka kuzama
ardhini bila sababu.
Polisi wilayani Kahama imethibitisha kuwa inawashikilia watu hao.




No comments:
Post a Comment