Hayo yalisemwa na JK mwenyewe katika hotuba aliyoitoa ikulu Machi 31,
2013 ambayo ni utaratibu aliojiwekea wa kuwahutubia Watanzania kila
mwisho wa mwezi.
JK alikuwa akijibu tuhuma zinazoelekezwa kwake
kutoka pande zote za dini ya Kiislam na Kikristo kwamba amekuwa
akipendelea upande mwingine.
Akizungumza bila kumung’unya maneno lakini katika hali iliyoonesha kusikitishwa na madai hayo, JK alisema:
“Ndugu
wananchi, nyaraka na kauli kalikali zinazotolewa na viongozi wa dini za
Kikristo na Kiislam zinanishawishi kuamini haya niyasemayo. Nyaraka na
kauli hizo zina mambo mawili makuu.
“Kwanza, kwamba kila upande
unatuhumu, kushutumu na kulaumu upande mwingine kwa kufanya vitendo
viovu dhidi ya dini yake. Kauli na mihadhara ya kudhalilisha dini za
wengine, kunajisi vitabu vitakatifu, kuchoma moto nyumba za ibada, mzozo
kuhusu nani achinje na kuuawa kwa viongozi wa dini ni baadhi ya mambo
yanayotolewa mifano.
“Na pili kwamba, kila upande unailaumu serikali
kwa kupendelea upande mwingine. Wakristo wanalaumu kwamba mihadhara ya
kudhalilisha Ukristo inaendeshwa na serikali haichukui hatua. Aidha,
Wakristo wanateswa na viongozi wao kuuawa na Waislam lakini serikali
haichukui hatua.
“Kwa ajili hiyo wanadai kuwa serikali imeshindwa
kulinda uhai wa raia wake. Wanasema pia kwamba serikali inapendelea
upande wa Waislam.
“Waislam nao wanadai kuwa kitabu chao kitakatifu, yaani Quran Tukufu, kinadhalilishwa kwa kuchanwa, kuchomwa moto na kukojolewa na Wakristo na serikali haichukui hatua yoyote ya maana. Waislam wananyanyaswa katika nchi yao, wanakamatwa hovyo, hawapewi fursa sawa, na kwamba serikali inawapendelea Wakristo.

“Mimi binafsi
wananishutumu kuwa napendelea kushiriki zaidi shughuli za Wakristo
kuliko za Waislam kama vile harambee za kujenga makanisa na shule za
makanisa. Naambiwa kuwa mwepesi kushiriki maziko ya maaskofu kuliko
mashehe wanapofariki dunia.
“Ipo misikiti mitatu hapa Dar es Salaam wamenisomea itikafu nife. Katika itikafu hiyo wamewajumuisha Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ndugu Suleiman Kova.

wananchi, napenda kuwahakikishia Watanzania wenzangu kuwa mimi na
serikali ninayoiongoza, hatupendelei upande wowote. Hatufurahishwi na
kitendo cha mtu kudhalilisha dini ya mwenzake ndiyo maana wapo wahadhiri
wa dini ya Kiislam na wahubiri wa dini ya Kikristo wamekamatwa na
kufunguliwa mashtaka kwa nyakati mbalimbali,” alisema JK bila kuitaja
misikiti hiyo.
Hata hivyo, kuna madai kwamba, misikiti hiyo, mmoja upo Temeke, miwili ipo Kariakoo ambapo waumini wake wamewahi kukesha kwa ajili ya dua ya Itikafu kwa viongozi hao jambo ambalo rais amekanusha kuangamiza imani yoyote nchini.

No comments:
Post a Comment