EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, April 4, 2013

KUPOROMOKA KWA GHOROFA DAR, UWT YATOA TAMKO.

 
Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi.
Yaomba hatua zinazochukuliwa ziwe endelevu kukomesha majanga ya kizembe
NA MWANDISHI WETU
UMOJA wa Wanawake wa Tanzania (UWT) umelezea kusikitishwa  kwake na matukio ya watu kupoteza maisha na kujeruhiwa yaliyotokea hivi karibuni, likiwemo la kuporomoka jengo la ghorofa 16, jijini  Dar es Salaam, na kusababisha vifo vya watu 36 na kujeruhiwa wengine kadhaa.
 
Tukio lingine ni lililotokea juzi, Aprili mosi, ambako watu zaidi ya watu 20 wameelezwa kupoteza maisha baada ya kuangukiwa na kifusi katika machimbo ya Moramu, eneo la Chekereni mkoani Arusha.
Katika taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya UWT jijini Dar es Salaam,  leo, Aprili 3, 2013, 

Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo, Amina Makilagi amesema, UWT pia inalaani matukio ya kuchinjwa kwa wanawake yanayoendelea kutokea Wilaya ya Butiama Mkoa wa Mara ambapo taarifa zilizopo Mwanamke mmoja amechinjwa kinyama kwa kutenganishwa kichwa na kiwiliwili chake na watu wasiojulikana.

"UWT imesikitishwa na vitendo vya kinyama vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio  na moyo wa kibinadamu kwa kuwakata vichwa wanawake na kuondoka navyo kwa malengo yao binafsi hivyo kusababisha wanawake kuishi katika maisha ya wasiwasi katika nchi yao", alisema Amina katika taarifa hiyo.
Alisema, UWT inaungana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete  kwa kutoa maelekezo mazito kwa mamlaka husika kuchukua hatua kali kwa wahusika wa matukio yote.
 
Hata hivyo UWT imeomba hatua zinazochukuliwa na serikali dhidi ya majanga hayo, ikiwemo kuporomoka kwa ghorofa, watu kuangukiwa na kifusi kwenye machimbo na watu kukatwa vichwa, ziwe hatua endelevu kuhakikisha matukio hayo hayatokei tena kirahisi.
"UWT pamoja na kutambua hatua za awali zilizochukuliwa hadi sasa katika matukio hayo, inaiomba Serikali kuhakikisha hatua inazochukua sasa ziwe ni endelevu ili kuhakikisha matukio kama haya ambayo kwa sehemu kubwa yanatokana na uzembe hayatokei tena", alisema Makilagi katika taarifa hiyo na kuongeza;-
 
"UWT inaungana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Kikwete kwa kutoa maelekezo mazito kwa mamlaka husika kuchukua hatua kali kwa wahusika wa matukio yote".
Amina aliwaombea ndugu jamaa na marafiki wa marehemu kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya wapendwa wao ambao wameacha pengo katika familia zao na Taifa kwa ujumla na kuwaombea wapone haraka waliojeruhiwa.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate