EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, April 4, 2013

Kupanda nauli kwazua balaa wananchi wapinga.

Dar es Salaam. 
Siku moja baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchikavu (Sumatra), kutangaza kupandisha nauli za daladala, mabasi ya kwenda mikoani, usafiri wa reli na tozo za majini kuanzia Aprili 12, baadhi ya wabunge, wanasiasa, wasomi, wanaharakati na wananchi wa kawaida wamesema hatua hiyo ni ya kuwaongezea wananchi ugumu wa maisha.
 

Juzi, Sumatra ilisema nauli hizo zimeongezeka kwa kiwango cha asilimia 24.46 na kwamba hatua hiyo imezingatia maoni ya wadau na gharama za uendeshaji.
 

Wakati Sumatra ikilaumiwa kwa kupandisha nauli hizo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema chama hicho kimeunda kikosikazi kwa ajili ya kupitia takwimu ilizotumiwa na wadau kupandisha nauli, baadaye kitatoa msimamo wake, ikiwa ni pamoja na kuishauri Serikali.
 

Kwa upande wake, Mbunge wa Tunduru, Mtutura Mtutura (CCM) alisema muda wa kupandisha nauli haujafika kwa kuwa bei ya mafuta haijapanda.“Hakuna sababu ya kupandisha nauli kwa wakati huu kwa sababu hata gharama za uendeshaji ziko palepale,” alisema Mtutura.
 

“Wanaomiliki mabasi watueleze kama wameajiri wafanyakazi au wanalazimisha tu mambo,” alisisitiza mbunge huyo.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alisema si muda wa mwafaka kwa wamiliki wa mabasi kupandisha nauli na kwamba hatua hiyo, itaathiri nchi kiuchumi.
“Itaongeza gharama za maisha na mfumuko wa bei. Lakini itawaumiza wananchi wa kipato cha chini,” alisema Zitto.


Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Peter Serukamba, alisema anafuatilia ili kujua sababu za Sumatra kupandisha nauli na kwamba atatoa taarifa atakapozipata.
Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza alisema kupanda kwa nauli kulitarajiwa kutokana na hali halisi ilivyo sasa.
“Ila sina uhakika kama Serikali imejipanga vyema kuwasaidia wananchi maskini,” alisema mtendaji huyo wa NCCR- Mageuzi.
Ruhuza alisema wananchi wa kawaida, watakabiliwa na wakati mgumu na kwamba ili kulimaliza tatizo hilo, Serikali inapaswa kujipanga.


Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Bashiru Ally alisema kupanda kwa nauli hizo, kutawaumiza zaidi walalahoi hasa ikizingatiwa kuwa hivi sasa kila kitu kipo juu. Vitu hivyo vinajumuisha kodi ya nyumba, gharama za matumizi ya maji, umeme na vyakula.


“Nchi yetu hivi sasa haina magari ya umma ambayo tungeweza kusema kuwa nauli yake ingekuwa nafuu. Hii inaonyesha kuwa nchi yetu inabaki kuwa na matabaka na walio hoi wataendelea kuwa hoi kwa kuwa hakuna juhudi zinazofanywa ili kuwainua,” alisema Bashiru.


Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Helen-Kijo Bisimba alisema nauli zinapanda wakati wafanyakazi wakiendelea kulipwa mishahara midogo, jambo linalowafanya wazidi kuishi maisha magumu.


“Nadhani Serikali ingepitia upya viwango vya mishahara kwa watumishi wake, ili waweze kumudu gharama za maisha kwa kuwa hivi sasa kila kitu kipo juu,” alisema Bisimba. Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro alisema kupanda kwa nauli hizo kunajenga taifa la wananchi wanaokabiliwa na hali ngumu katika kila sekta.


“Mfano nauli za mikoani zimepanda bila huduma kuboreshwa, binafsi nadhani hiyo ilikuwa hoja ya msingi ya Sumatra kukataa kupandisha nauli hizo, Watanzania ni maskini na tunajua wazi kuwa hivi sasa kila kitu bei yake ni juu, leo tena nauli zimepanda, hapa tunatengeneza taifa la walalahoi,” alisema Mtatiro.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate