EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, April 4, 2013

Vurugu za hatari zazuka Tunduma kuhusu nani anayepaswa kuchinja mifugo baina ya waumini wa dini mbili; Waislamu na Wakristo.

Tunduma. 
Vurugu kubwa zilizuka jana katika Mji wa Tunduma ambao ni makao makuu ya Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, baada kutokea mvutano mkali kuhusu nani anayepaswa kuchinja mifugo baina ya waumini wa dini mbili; Waislamu na Wakristo.


Mamia ya polisi kutoka wilaya zinazouzunguka Mji wa Tunduma walimwagwa na walilazimika kutumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha ili kuwatawanya waandamanaji pia, kutuliza vurugu zilizodumu kwa zaidi ya saa nne.

Vurugu hizo ambazo zinahatarisha amani, zimetokea siku tatu tu tangu Rais Jakaya Kikwete aonye kwamba kwamba vurugu zenye sura ya kidini ni hatari na zinaweza kuvuruga amani na utulivu uliodumu kwa miaka mingi nchini.


Mijadala kuhusu vurugu hizo ilitawala katika mitandao ya kijamii ikiwamo facebook, Mabadiliko Forum na Jamii Forums ambako watu mbalimbali walionyesha kukerwa nazo, huku wakiitaka Serikali ichukue hatua za kudhibiti.



Kutokana na vurugu hizo zilizoanza saa 4:30 asubuhi, wakazi wa mji huo walijifungia ndani kwa kuhofia usalama wa maisha yao, huku maduka na shughuli za biashara nazo zikifungwa.
Mwandishi wa Mwananchi aliyekuwa katika eneo la tukio anaripoti kwamba katika vurugu hizo, watu zaidi ya 35 wamekamatwa wakiwamo Diwani wa Kata ya Tunduma Frank Mwakajoka na Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Gidion Mwamafupa.


Habari zaidi zinasema barabara za mji huo zilifungwa, umeme ulizimika baada ya moto kulipuka kwenye moja ya nguzo za umeme. Pia mpaka wa Tanzania na Zambia ulifungwa kwa muda.


Magari ya abiria na yale ya usafirishaji yaliyokuwa yakitoka na kuelekea Zambia, Dar es Salaam, Sumbawanga na Mbeya Mjini pia yalikwama na kusababisha usumbufu mkubwa kwa abiria. Msikiti ulivunjwa na watu wawili akiwamo askari polisi walijeruhiwa.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kwamba tukio hilo limetokea wakati Serikali ikiwa kwenye mazungumzo na baadhi ya wahusika katika mgogoro wakiwamo viongozi wa dini na wachinjaji wa nyama.


“Mgogoro wa kuchinja umedumu kwa siku tatu, jana kamati ya ulinzi na usalama chini ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ilikutana na baadhi ya viongozi wa dini na wadau wa kuchinja nyama na kuna mambo matatu ambayo yalitolewa katika mkutano huo,” alisema Diwani.


Alisema katika mkutano huo Kandoro aliagiza kuwa wananchi wanatakiwa kuwa wavumilivu katika kipindi hiki, ambacho Serikali ngazi ya kitaifa inalishughulikia na kuwataka kuendelea na hali uchinjaji kama ilivyokuwa awali na kila mmoja afanye kile anachoamini katika dini yake wakati wa kula.


Hata hivyo, baadhi ya Wakristo waliafikia lakini wengine hawakuafiki. Hivyo jana asubuhi walihamasisha maandamano katika mji huo ambayo yalisababisha vurugu hizo.


“Pamoja na hayo yote uchunguzi wa kitaalamu tumebaini kuwa vurugu hizo siyo za kidini, bali zimehusishwa siasa kwani hata viongozi wa dini waliohusika ni baadhi siyo wote ambao wanajishughulisha na suala hili,” alisema Diwani.Alisema kwa upande mwingine vurugu hizo zinafanywa na baadhi ya vijana wenye nia ya kuzitumia kwa lengo la kufanya uporaji.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate