
Tukio hilo lilitokea Jumatatu iliyopita saa tatu na robo usiku ambapo
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki
amethibitisha na kuwataja marehemu kuwa ni Asia Yahya (52), wanafunzi wa
Shule ya Msingi Ilonga, Abubakari Yahaya (8) na Fatuma Yahaya (6).

Kamanda
Masaki ameongeza kuwa ajali hiyo ilihusisha malori mawili yaliyogongana
kisha moja kugonga nyumba na kusababisha vifo vya watu hao na majeruhi
ambao ni Abuu Fadhil (22) na Steven Chiwa (26) ambao wamelazwa katika
Hospitali ya Misheni ya Chimala.

Alisema
chanzo cha ajali ni gari lenye namba za usajili T578 ALS likiwa na tela
lenye namba za usajili T125 AGM aina ya Scania kuligonga kwa nyuma
gari lenye namba T959 ASC ambalo pia ni aina ya Scania.

Alisema gari namba T959 ASC lilikuwa likiendeshwa na Juhudi Saimon
(34), mkazi wa Dar es Salaam na ndilo lililogonga nyumba, mali ya Matia
Mwagala mkazi wa Kijiji cha Ilongo ambayo marehemu walikuwa ndani.

Hata hivyo, dereva wa gari lililosababisha ajali alikimbia na gari mara
baada ya tukio ambapo Kaimu Kamanda anatoa rai kwa yeyote mwenye
taarifa juu ya mahali alipo dereva wa gari lililosababisha ajali hiyo
atoe taarifa kwani anatafutwa na polisi.
(PICHA NA MBEYA YETU)
No comments:
Post a Comment