EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, April 3, 2013

Lowassa amtoa kafara Pinda.

Wabunge waunganisha nguvu kutaka kumsulubu bungeni
RIPOTI ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa mwaka 2006 kuchunguza ujenzi wa maghorofa katika Jiji la Dar es Salaam, imemweka mahala pabaya na inaweza kumtoa kafara, Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo Pinda, Tanzania Daima Jumatano limedokezwa.

Pinda anatolewa kafara katika sakata la jengo la ghorofa 16 lililoporomoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam wiki iliyopita na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 40.
Kutokana na janga hilo, Pinda analalamikiwa kukalia ripoti ya Tume ya Lowassa ambayo ilikuja na mapendekezo ya kukabiliana na maghorofa yaliyojengwa chini ya kiwango.

Duru za siasa kutoka ndani ya Bunge zinasema kuwa tayari kuna baadhi ya wabunge bila kujali itikadi zao, wameunganisha nguvu kutaka kumsulubu Waziri Pinda katika mkutano ujao wa Bunge kupitia hoja binafsi au maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu.
Mmoja wa mawaziri waandamizi wa serikali ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema: “Pinda anastahili kubeba mzigo, kwani baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo alimwajibisha nani tangu 2008 hadi sasa?

“Kwa uzembe huu, Pinda ameshiriki kwa kuwa hakuwawajibisha waliojenga kinyume na utaratibu hadi Watanzania wengine wakafa. Zamu hii hata akilia anahusika.” Mbunge wa Vunjo Augustino Mrema (TLP) alimshangaa Waziri Pinda kwa kushindwa kuchukua hatua zilizopendekezwa na tume ya Lowassa kwani ilipendekeza baadhi ya majengo yabomolewe na wahusika wachukuliwe hatua.
Alisema athari ya ukimya huo ni kuendelea kuangamia kwa Watanzania kunakosababishwa na uzembe wa viongozi wa serikali.

“Hili tatizo la kushindwa kuchukua uamuzi mgumu litaendelea kutugharimu kila siku, yale maghorofa yaliyotakiwa kubomolewa kipindi kile hayajaguswa na hayataguswa kwa sababu ya kubebana, hili hatuwezi kulinyamazia, lazima tukawashe moto bungeni,” alisema Mrema.
Alisema Watanzania hawapo tayari kuletewa danganya toto ya tume nyingine ikalete majibu ambayo tayari yako mezani kwa Pinda.

Mbunge wa CCM aliyeomba jina lake lihifadhiwe, alisema kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata watendaji wa Manispaa ya Ilala hakitoshi kama Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ataendelea kubaki ofisini.
Mrema ambaye amepata kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani kwa nyakati tofauti, alisisitiza kuwa Waziri Tibaijuka anapaswa aige mfano wa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Lowassa walioamua kuachia ngazi kutokana na uzembe wa watendaji wao.

“Kwa wenzetu leo inapotokea boti ikazama kwa uzembe na kupoteza maisha ya watu watatu waziri mwenye dhamana anawajibika, iweje sisi leo tuwachekee mawaziri wetu?” alihoji mbunge huyo.

Mbunge wa kuteuliwa na rais, James Mbatia, ameapa kuwasha moto katika Bunge lijalo hadi kieleweke.

Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema lazima Waziri Mkuu atoe majibu ya msingi kwa Watanzania kwanini hakutekeleza maazimio ya tume ya Lowassa.

Alienda mbali na kuhoji utendaji wa kitengo cha maafa cha Waziri Mkuu kwani kimekuwa kikishughulika kutoa vyakula vya misaada kwenye maafa badala ya kudhibiti yasitokee.
“Tangu tume zianze kuundwa kuhusu maafa ni akina nani walichukuliwa hatua? Kuanzia tume ya MV Bukoba hadi tume ya matokeo ya kidato cha nne, Watanzania tumechoka kuneemesha mifuko ya wajumbe wa tume na kufilisi rasilimali zetu, hivyo Pinda, Tibaijuka lazima wajiuzulu,” alisema.

Wakati wabunge hao wakitaka Pinda na Tibaijuka waachie ngazi, habari zaidi ndani ya serikali zinasema kuwa ripoti ya Tume ya Lowassa haikufanyiwa kazi kwani baadhi ya majengo yaliyopendekezwa kubomolewa, yanawahusu viongozi wa juu serikalini.
“Ile ripoti iliwasilishwa wakati Lowassa bado yuko madarakani. Alishindwa kuifanyia kazi na haiwezi kufanyiwa kazi kwani baadhi ya majengo yanawahusu viongozi au yanamilikiwa na watu wa karibu wa viongozi, na ndio wachangiaji wakubwa wa fedha wakati wa kampeni,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Akifanya majumuisho katika hotuba ya matumizi ya ofisi yake bungeni kwa mwaka 2008/09, Pinda alizungumzia jinsi Tume ya Lowassa ilivyofanya kazi katika sakata la ghorofa kuanguka jijini Dar es Salaam.
Pinda alilithibitishia Bunge kuwa zaidi ya maghorofa 100 jijini Dar es Salaam yalibainika kuwa yalijengwa kinyume na taratibu za ujenzi.
Kwa mujibu wa ripoti iliyoundwa na Lowassa, kati ya maghorofa 505 ambayo waliyakagua, 147 yalikutwa hayana nyaraka za ujenzi.

Lowassa aliunda tume baada ya jengo la hoteli ya Chang’ombe Village Inn, Keko, Dar es Salaam kuanguka mwaka 2006 na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa. Ilidaiwa kwamba ulikuwapo ukiukwaji katika ujenzi wake.
Pinda aliliambia Bunge kuwa tume hiyo ya Lowassa ilibaini pia maghorofa 81 yalikutwa yamekiuka masharti ya ujenzi huku mengine 22 wenyewe hawakupatikana na yalikuwa yamejengwa bila kuzingatia sheria za ujenzi pamoja na uzembe wa baadhi ya watendaji wakiwamo wahandisi wa manispaa husika.

NHC yatoa kauli
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limesema kuwa mbia wao alikuwa na vibali vya mamlaka zinazohusika kusimamia ujenzi wa majengo makubwa vya kumruhusu kuongeza ghorofa 16 kutoka kumi za awali.
Kauli hiyo inakuja kukiwepo na mvutano kutoka mamlaka mbalimbali ikiwemo Manispaa ya Ilala kwamba mbia wao huyo ambaye ni M/s Ladha Construction alipewa kibali cha kujenga ghorofa kumi, lakini cha kushangaza aliongeza nyingine sita bila taarifa na hivyo kusadikiwa kuwa huenda ndiyo chanzo cha kuanguka kwa jengo hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa NHC, Nehemiah Mchechu akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaa, alisema Agosti 22 mwaka jana mbia wao huyo aliwataarifu kuwa ameshapata vibali kutoka mamlaka husika, na kwamba angependa aingie nao mkataba mdogo kutambua ongezeko la ghorofa hizo na mabadiliko ya tarehe ya kumaliza mradi.
“Shirika lilimjibu kuwa hakuna pingamizi kama mbia ataleta nakala ya vibali kutoka mamlaka husika kwa ajili ya kumbukumbu za shirika na pia ili kufikia hatua za maamuzi ya ndani na mawasiliano yote hayo yapo kwenye rekodi zetu na endapo mamlaka husika itazihitaji tuzazipatia,” alisema.
Kutokana na hali hiyo, aliutaka umma kutoliingiza shirika hilo katika sakata hilo kwa madai kuwa zipo taasisi na vyombo vinavyokasimiwa mamlaka ya kusimamia ubora wa ujenzi wa nyumba nchini, na NHC nayo husimamiwa na taasisi na vyombo hivyo.
CHANZO TANZANIA DAIMA

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate