Sumbawanga.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke, mkazi wa kitongoji cha Chemka ,Kata ya Chanji Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa amejikuta akipata uchungu wa ghafla na kujifungua mtoto wa kiume chooni, nyumbani kwake kutokana na mshtuko alioupata baada ya kutolewa kwa nguvu katika nyumba hiyo na dalali wa mahakama.

Katika tukio hilo ambalo mwanamke huyo (jina linahifadhiwa) alipata mshtuko mkubwa baada ya dalali wa mahakama kufika nyumbani kwake na kuanza kutoa nje vyombo vyake vyote kwa madai kuwa nyumba hiyo ilikuwa na mgogoro.
Kwa mujibu wa mwanamke huyo baada ya dalali kuwatoa kwa nguvu katika nyumba hiyo kwa kutoa nyombo vyao vyote nje na kufunga nyumba hiyo kwa makufuli baada ya kuhaha na kukosa sehemu ya kuhifadhi vyombo hivyo yeye na familia yake walilazimika kulala nje ya nyumba hiyo na kunyeshewa na mvua usiku kucha.
Alisema baada ya kutaabika usiku kucha kwa
kunyeshewa na mvua ilipofika saa tano asubuhi alibanwa na uchungu
mkali alipolazimika kukimbilia chooni na kujifungua mtoto wa kiume
akiwa hai.
No comments:
Post a Comment