Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akiwasili eneo la ajali.
Mwili wa
dereva wa lori moja kubwa lenye ujazo wa tani 18 ukiwa umeopolewa na
askari jeshi, tayari kupelekwa mochwari ya Hospitali ya Mt Meru. Dereva
huyu ametambulika kwa jina moja tu la Alex amefikwa na mauti akiwa ndani
ya gari hilo wakati vijana wengine wakiendelea kupakia moram asubuhi ya
leo
Baadhi
ya wananchi waliojitokeza kushuhudia ajali hiyo mbaya wakishangaa zoezi
la uokoaji na wengine wakisubiri kutambua ndugu zao, jambo ambalo
halikupata nafasi
Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh Gaudence Lyimo akisaidiana na vikozi vya jeshi katika zoezi la uokozi.
Mh Lema akiangalia namna vikosi vya Jeshi la Wananchi pamoja na askari Polisi wakiendelea na zoezi la uokozi.
Mwananchi huyu aliishiwa nguvu baada ya kushuhudia mwili wa rafiki yake ukiopolewa kutoka kwenye kifusi.
Hali ilivyo machimboni hapo
Kina mama wakilia kwa uchungu wakihofu kuondokewa na wapendwa wao
Vikosi vya Jeshi la Wananchi na Polisi vikiwa kazini
Sehemu ndogo ya Fuso ikionekana huku gari nyingine ikiwa haionekani kabisa
Ambulance ya Jiji tayari tayari kwa lolote ikihitajika
Wachina wakielekea eneo la jali na vifaa vyao kusaidia zaidi zoezi la uokozi
Wanajeshi zaidi wakielekea chini kwenye mgodi
Tunaomba radhi kwa ubora hafifu wa picha hizi….
KWA
mujibu wa mashuhuda wa ajali iliyotokea leo asubuhi Jijini Arusha,
inakadiriwa zaidi ya watu 18 wamepoteza maisha kufuatia kufukiwa na gema
la mchanga/moram wakati wakichimba na kupakia kwenye malori.
Ajali
hiyo mbaya imetokea katika machimbo ya moram nje kidogo ya Jiji eneo
jirani na Moshono-Kiserian ambapo vijana hao wanaokadiriwa kufikia idadi
hiyo walikuwa wakipakia moram kwenye magari mawili, moja ni Fuso na
lingine kubwa zaidi (tani 18) na yote mawili yamefukiwa kabisa na
kifusi.
Vilio toka kwa kina mama huku baadhi wa wababa na marafiki na ndugu wa jamaa waliofukiwa wakishindwa kujizuia na kuangua kilio.
Meya wa Manispaa Mh Gaudence Lyimo pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema ni miongoni mwa viongozi wakubwa waliofika eneo la ajali kusaidiana na kikosi cha Jeshi la Wananchi kufanya uokozi.
CHANZO CHA HABARI NI 2JIACHIE- www.2jiachie.com
No comments:
Post a Comment