MAMILIONI ya fedha za benki za NMB na CRDB yalinusurika kuibwa jana
baada ya majambazi wasiofahamika idadi kubomoa ukuta wa mashine mbili za
kutolea fedha (ATM) eneo la Tabata Kimanga Dar es Salaam. Tukio hilo
lilitokea usiku wa kuamkia jana wakati majambazi hao wakiwa na mitungi
ya gesi walipoingia ndani ya ATM hizo na kuanza kuyeyusha baadhi ya
vyuma kwa lengo la kufika zilipohifadhiwa fedha.
Kutokana na uimara wa sehemu zinapohifadhiwa fedha kwenye ATM, majambazi hao hawakuweza kufanikiwa kuchukua fedha hizo.
Kutokana na uimara wa sehemu zinapohifadhiwa fedha kwenye ATM, majambazi hao hawakuweza kufanikiwa kuchukua fedha hizo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala,
Marietha Komba alisema majambazi kabla ya kuanza shughuli ya kubomoa
ukuta waliwateka walinzi wawili waliokuwapo na kuwapulizia dawa kitendo
ambacho kiliwafanya washindwe kujitambua.
Alisema walinzi hao ni Abdallah Ally kutoka Kampuni ya Ulinzi ya Moto ambaye aliyekuwa mlizi wa ATM ya NMB na Bakari Gabriel kutoka Kampuni ya Ulinzi ya Ultimate aliyekuwa mlinzi wa ATM ya CRDB.
“Ni kweli majambazi yamevamia ATM mbili za NMB na CRDB zilizo Tabata Kimanga na wameweza kutoboa ukuta na kuingia ndani na kuanza kuyeyusha baadhi ya vyuma palipo hifadhiwa fedha.

“Lakini hawakufanikiwa kuchukua hata senti moja kutokana na uimara wa sehemu panapohifadhiwa fedha hizo.
“Katika hili tunashukuru utaalamu unaotumika katika kujenga ATM za fedha kwa sababu wangefanikiwa kuchukua mamilioni ya fedha za watu,” alisema.
No comments:
Post a Comment