Arusha.
Mataifa ya Afrika ya Mashariki (EAC), yamekubaliana kuwa na mkakati wa pamoja kwa kukuza uchumi, kwa kutumia rasilimali ambazo zimegundulika katika nchi hizo kama mafuta, gesi na madini.
Mataifa ya Afrika ya Mashariki (EAC), yamekubaliana kuwa na mkakati wa pamoja kwa kukuza uchumi, kwa kutumia rasilimali ambazo zimegundulika katika nchi hizo kama mafuta, gesi na madini.
Rais Jakaya Kikwete akiwa na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (kushoto) na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni baada ya kumalizika kwa mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Arusha jana. Picha na Filbert Rweyemamu
Mwenyekiti wa Marais wa nchi za Afrika ya Mashariki, Yoweri Museven aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa 11 wa wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki uliofanyika kwenye Hoteli ya Ngurdoto mkoani hapa.
Rais Museven alisema, rasilimali zilizogundulika sasa katika nchi za Afrika ya Mashariki, zikitumiwa vizuri zinaweza kuzifanya nchi zote za Afrika ya Mashariki kutoka katika nchi zinazoendelea kuwa nchi zilizoendelea ifikapo mwaka 2063.
Awali, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema nchi za Afrika Mashariki, pia zinaweza kuendelea kwa kasi, kama zikifufua mipango ya pamoja ya kuboresha sekta ya Miundo mbinu, ikiwamo ya usafiri wa reli, barabara na bandari.
Kenyatta ambaye jana ilikuwa mara yake ya kwanza
kuhutubia kikao cha Marais na
Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki , kama Rais wa Jamhuri ya Kenya ,alisema miradi ya pamoja katika nchi za Afrika ya Mashariki, kutasaidia sana kukuza uchumi kwa kasi kwa kila nchi badala ya kila nchi kuendeleza mradi wake.

“Tunahitajika kufanyakazi kwa pamoja katika
kuendeleza miradi mbalimbali na hapo ndipo tutawavutia wawekezaji na
hivyo kuinua hali ya uchumi”alisema Kinyatta
Katika mkutano huo, Marais wanne,waliohudhuria, walijadili itifaki ya umoja wa fedha katika nchi za Afrika ya Mashariki, kabla ya kutiwa saini Novemba mwaka huu.
Katika mkutano huo, Marais wanne,waliohudhuria, walijadili itifaki ya umoja wa fedha katika nchi za Afrika ya Mashariki, kabla ya kutiwa saini Novemba mwaka huu.
Marais hao, Museveni wa Uganda, Jakaya Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pierre Ngurunziza wa BurundI na
Uhuru Kenyatta wa Kenya, pia waliwaapisha Naibu Katibu Mkuu wa
Jumuiya ya Afrika ya Mashariki,kutoka Kenya, Charles Njoroge ambaye
anachukuwa nafasi ya Dk Julius Rotich aliyemaliza muda wake.
Marais hao, pia waliwaapisha majaji wawili, wa Mahakama ya Afrika ya Mashariki.
No comments:
Post a Comment