LAURENCIA Lushulwan'hambi (36)mkazi wa Kijiji cha Busolwa Wilaya ya
Nyang'hwale mkoani Geita ambaye alikuwa anashikiliwa katika Kituo cha
Polisi Kharumwa akituhumiwa kwa mauaji, anadaiwa kutoroka katika
mazingira ya kutatanisha.
Inadaiwa mwanamke huyo alitoroka Machi 20 mwaka huu wakati askari waliokuwa zamu wakimuandalia shitaka la mauaji ya mwanamke mwenzake, Pili Thobias (33) mkazi wa Kijiji cha Busolwa, baada ya kutokea ugomvi baina yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Leonard Paulo alikiri kutoroka kwa mtuhumiwa huyo akidai jeshi la polisi linaendelea kumsaka mwanamke huyo kuhakikisha anafikishwa katika vyombo vya sheria. Alisema uchunguzi dhidi ya polisi waliozembea na kusababisha mwanamke huyo kutoroka unaendelea na hatua za sheria zitachukuliwa dhidi ya askari hao walioshindwa kuzingatia majukumu yao.
"Mazingira ya kituo cha
wilaya yamechangia kutoroka kwake…hata nyinyi (waandihsi wa habari)
mnayafahamu mazingira ya kituo hicho.Inadaiwa mwanamke huyo alitoroka Machi 20 mwaka huu wakati askari waliokuwa zamu wakimuandalia shitaka la mauaji ya mwanamke mwenzake, Pili Thobias (33) mkazi wa Kijiji cha Busolwa, baada ya kutokea ugomvi baina yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Leonard Paulo alikiri kutoroka kwa mtuhumiwa huyo akidai jeshi la polisi linaendelea kumsaka mwanamke huyo kuhakikisha anafikishwa katika vyombo vya sheria. Alisema uchunguzi dhidi ya polisi waliozembea na kusababisha mwanamke huyo kutoroka unaendelea na hatua za sheria zitachukuliwa dhidi ya askari hao walioshindwa kuzingatia majukumu yao.
“Lakini pamoja na hayo sisi tunachunguza uzembe wa askari waliosababisha mtuhumiwa huyo kukimbia," alisema Paul.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa Machi 19, mwaka huu kwa tuhuma za mauaji baada ya kumvamia Pili Thobias nyumbani kwake.
Inadaiwa mtuhumiwa alimvamia Pili nyumbani kwake kutokana na kuingilia ugomvi wa watoto wao ambako mtuhumiwa alimkamata mtoto wa Pili na kisha kuanza kumpa adhabu.
Pili alipozuia mwanae kupigwa alishambuliwa na kujeruhiwa vibaya za kifuani na shingo hali iliyosababisha apelekwe kwenye Kituo cha Afya cha Nyang'hwale kupatiwa matibabu.
Hata hivyo alihamishiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita ambako alifariki dunia siku moja baadaye.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Elija Jomo alisema wanawake hao walipigana Machi 17 mwaka huu baada ya watoto wao kugombana katika michezo yao ya utoto.
No comments:
Post a Comment