Dar es Salaam.
Mfanyabiashara na mkazi wa Kigamboni,
Dar es Salaam, Omary Maneno (36) na mkewe Judith Lucas ama Lea (28)
wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na
shtaka la kuwapiga watoto wao kwa kutumia fimbo na mabomba.
Akisoma
hati ya mashtaka jana, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumain Kweka
alidai kuwa Februari 2013, Maneno na mkewe Judith, ambaye ni mama wa
kambo wa watoto wa kike wenye umri wa miaka 7 na 5 waliwapiga kwa
kutumia fimbo na mabomba na kuwasababisha maumivu makali mwilini.
Ilidaiwa
kuwa washtakiwa hao walifanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 169
(1) na (2) cha sheria ya Kanuni ya Adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka
2002.
Iliendelea kudai kuwa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka saba
ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Bunge, Wilaya
ya Ilala wakati mdogo wake mwenye umri wa miaka mitano ni mwanafunzi wa
chekechea shuleni hapo.
Baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka hayo, walikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka hayo, walikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
No comments:
Post a Comment