Klabu za ligi kuu soka nchini
England zimepitisha sheria ya kutumia teknolojia ya camera katika
maamuzi ya mchezo wa soka kuanzia msimu ujao.
Kampuni ya Uingereza ya Hawk-Eye imeshinda tenda
na kupatiwa mkataba wa kufunga vifaa maalumu kwenye viwanja vyote 20
vya timu za ligi kuu nchini England.
Hawk-Eye
itafunga kamera saba kwenye kila goli maalumu kwa kutambua
kama mpira
umevuka mstari wa goli na kumjulisha mwamuzi wa mchezo huo kupitia saa
yake ya mkononi,na imesema inauhakika hakuna marejeo yoyote ya matangazo
ya picha ambayo yatapingana na maamuzi ya teknolojia hiyo.
Kampuni hiyo ya Hawk-Eye inajulikana kwa kufunga
teknolojia kama hiyo kwenye mchezo wa Tenesi na Kriketi,ambapo camera
maalumu huweza kutambua iwapo mpira umegusa mstari ama la na kumjulisha
mwamuzi na wasaidizi wake ndani ya sekunde chache.
Chama cha soka nchini England FA,kitafunga vifaa
hivyo kwenye uwanja wa Wembley tayari kwa kutumika kwenye mchezo wa
ngao ya jamii hapo mwezi wa nane mwaka huu.
Vilabu vikubwa vyote nchini England vimepiga
kura ya kupitisha maamuzi hayo katika mkutano wao uliofanyika hii leo
jijini London,Huku viwanja vingine vya timu 17 zitakazosalia ligi kuu na
zile 3 zitakazopanda daraja vitawekewa teknolojia hiyo na shughuli
nzima itachukua wiki sita kukamilika.
Msukumo wa kutumia teknolojia maalumu ya
kutambua goli ilipata nguvu baada England kukataliwa goli lao la
kusawazisha walipocheza na Ukraine,Mchezo ambao England walifungwa bao
moja kwa bila kwenye michuano ya kombe la mataifa barani Ulaya mwaka
2012, Ambapo mwezi mmoja baadaye bodi ya vyama vya soka vya kimataifa
(IFAB) katika kikao chake mjini Zurich kilipitisha teknolojia mbili ili
zitumike kwenye michezo ya soka.
Nalo shirikisho la kandanda Ulimwenguni FIFA
kupitia kwa rais wake Sepp Blater alisema kukataliwa kwa goli la Frank
Lampard kwenye mechi ya robo fainali kati ya England na Ujerumani mwaka
2010 katika michuano ya kombe la dunia,kulichangia kwa kiasi kikubwa
maamuzi ya shirikisho hilo kupitisha sheria ya matumizi ya teknolojia ya
kutambua goli.
Chama cha soka cha England kimesema kingependa kuona teknolojia hiyo inaanza kutumika kwa vitendo haraka iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment