Habari Na Prince Akbar
MSHAMBULIAJI
Mohamed Hussein, jioni ya jana ameinusuru Toto Africans kuzama mbele ya
Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro baada ya
kuifungia mabao mawili dakika za lala salama na kufanya sare ya 2-2
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Hadi
mapumziko, tayari Mtibwa Sugar walikuwa mbele kwa mabao mawili
yaliyowekwa kimiani na Juma Luzio dakika ya pili na Hassan Salum dakika
ya 14.
Wakati
dakika zikiyoyoma na Mtibwa wakiwa tayari wana matumaini ya kubeba
pointi tatu, Mohamed Hussein alicharuka ghafla na kufunga katika dakika
za 73 na 88.
Sare
hiyo, inaifanya Mtibwa ifikishe pointi 33 baada ya kucheza mechi 23 na
kuendelea kukaa nafasi ya tano nyuma ya Simba SC yenye 35, wakati Toto
inafikisha pointi 23 baada ya kucheza mechi 24 na inabaki nafasi ya 11.
Katika
mechi nyingine za ligi hiyo jana, Tanzania Prisons wameutumia vyema
Uwanja wa nyumbani, Sokoine mjini Mbeya kwa kuwalaza 1-0 JKT Mgambo, bao
pekee la Nurdin Issa dakika ya 14, wakati Polisi Morogoro imetoka sare
ya bila kufungana na Ruvu Shooting Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Ruvu
inabaki nafasi ya saba kwa pointi zake 30 baada ya kucheza mechi 21,
Mgambo inabaki nafasi ya tisa kwa pointi zake 24 baada ya kucheza mechi
22, Prisons inapanda kwa nafasi mbili hadi ya 10 kwa kufikisha pointi 23
baada ya kucheza mechi 23 na Polisi Moro inapanda kwa nafasi moja hadi
ya 13 baada ya kufikisha pointi 19, sawa na African Lyon inayoshika mkia
zikizidiana wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa tu.Via http://bongostaz.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment