Dodoma.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amelitaka Jeshi la Polisi mkoani Arusha kutumia busara katika kushughulikia suala la Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amelitaka Jeshi la Polisi mkoani Arusha kutumia busara katika kushughulikia suala la Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma
jana, Mbowe alisema kuwa kitendo kilichofanywa na polisi kuzunguka
nyumba ya Lema usiku na kutishia kupiga mabomu ya machozi ili
kumlazimisha mbunge huyo kutoka ndani, siyo cha busara na kinaweza
kuchochea hasira kwa wapigakura wake.
“Walizunguka nyumba ya mbunge usiku kama ya jambazi, kwa nini wanachokoza wananchi kwa ajili ya mtu mmoja? Haya mambo yakiendelea hivi watavuruga amani katika Mkoa wa Arusha,” alisema Mbowe akionya na kuongeza:
“Kibaya zaidi mpaka saa nne hii kabla hatujaanza mkutano huu hapa, naambiwa mbunge yupo ndani tu hawajamuhoji.”
Mbowe alieleza kuwa, kwa ushahidi uliopo ikiwa ni pamoja na video zilizopo kwenye mitandao ya kijamii unaoonyesha Lema akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ni dhahiri kuwa mbunge huyo hakufanya uchochezi wa aina yoyote.
“Lema alikuwepo nyumbani kwake siku zote na jana
(juzi) aliongea na waandishi wa habari. Hata siku ya tukio walisema
alikimbia, ukweli ni kwamba aliondoka pale na gari jingine baada ya
kuona polisi wameanza kurusha mabomu ya machozi na risasi,” alisema na
kuongeza:
“Kwa sababu anajua kuwa uhusiano wake na polisi Arusha siyo mzuri, mbunge aliamua kutafuta gari jingine ili atoke kwenye eneo lile wasije wakamdhuru. Alifanya hivyo kwa kuwa na yeye ni mjanja.”
Kutokana hali hiyo, aliitaka Serikali kumaliza kwa
busara suala hilo la Arusha bila kuweka itikadi za kisiasa. “Hatulizuii
Jeshi la Polisi kufanya kazi yake ni vyema tukatenga siasa na utendaji,
tuache pia kuweka mambo binafsi kwenye masuala kama haya,” alisema.
Wakati huohuo, mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei ameeleza kushangazwa na hatua ya polisi kumkamata Lema huku akisema kwamba nchi itakwenda kulipuka hivi karibuni kutokana na vuguvugu la watu kutaka haki zao za msingi. Mtei alisema ni ajabu kumkamata mtu ambaye alikuwa akiwatuliza wanafunzi huku akidai kitendo cha kumkamata ni ukandamizaji mkubwa wa haki za binadamu.
Alisema kuwa nchi italipuka kwa vurugu kama watu watazuiwa kudai haki zao huku akiwataka watawala kusoma alama za nyakati.
No comments:
Post a Comment